Home BIASHARA Waziri Jenister Mhagama akoshwa na Mshikofasta ya NMB

Waziri Jenister Mhagama akoshwa na Mshikofasta ya NMB

Google search engine
 Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya kaskazini, Baraka Ladislaus (kulia) alipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa Wilayani Babati, Manyara.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama (wapili kushoto) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya kaskazini, Baraka Ladislaus (wapili kulia) alipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa Wilayani Babati, Manyara. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la Babati, Antipas Nnko na kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako

Na MWANDISHI WETU

-MANYARA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama (Mb) amewataka vijana kuchangamkia fursa ya mkopo wa Mshikofasta inayotolewa na benki ya NMB katika kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo mkoani Manyara kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa yaliyoanza Oktoba 8 na yatafikia tamati Oktoba 14,2023 Wilayani Babati alipotembelea banda la benki ya NMB.

Waziri Mhagama alisema kuwa mkopo wa mshikofasta inayotolewa na benki ya NMB, umejipambanua katika malengo makubwa ya maadhimisho hayo ambayo ni kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira.

“Nimependa hiyo huduma ya mshikofasta na niwaombe vijana wachangamkie hiyo fursa na ninyi viongozi wa vijana wahamasisheni wananchi kuzitumia katika kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi” ameeleza Waziri Mhagama ambae pia aliambatana na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako.

Awali akimueleza Waziri Mhagama, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya kaskazini, Baraka Ladislaus amesema wamefikia kubuni huduma hiyo ya mkopo waliyoiita ‘mshikofasta’ kwa ajili ya kuwarahisishia wateja wao wanaofanya shughuli za kiujasiriamali kupata fedha za haraka kupitia simu zao za mkononi.

“Huduma hii unalenga kuwasaidia wajasiriamali kupata mkopo wa haraka kupitia simu zao za mkononi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kila siku. Mteja wa Benki ya NMB ataweza kukopa mpaka shilingi 500,000 bila kufika tawini na wala kuweka dhamana yeyote,” amesema Baraka

Akitoa salamu za Benki ya NMB katika uzinduzi wa wiki Meneja huyo wa Kanda alielezea juu ya uwepo wa masuluhisho mbalimbali kutoka benki ya NMB ambayo yanalenga vijana na kutumia nafasi hiyo pia kuwahamasisha vijana kutumia huduma hizo kwaajili ya kunufaika zaidi.

“Tunayo Huduma ya Spend to save ambayo inahamasisha uwekaji wa akiba, lakini pia tunaendelea kuwakaribisha vijana waweze kuwekeza kupitia hati fungani yetu ya Jamii bond yenye riba nzuri ya asilimia 9.5 kwa mwaka kwa manufaa yao ya baadae,” Alisema Meneja huyo.

Aidha, Meneja huyo ameeleza utayari wa Benki ya NMB katika kuendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wanawawezesha vijana na kuweza kujikwamua zaidi kiuchumi. Na pia kueleza shukrani za benki ya NMB kwa ushirikiano mwema wanaopata kutoka kwa serikali ya Mkoa wa Manyara na Serikali kuu kwa ujumla.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuwawezesha vijana kupata jukwaa la kujadili fursa zinazozotolewa na serikali na kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira.

Mmoja wa wajasiriamali vijana aliyehudhuria maonyesho hayo, Eva Martine amesema kuwa mkopo huo wa Mshikofast wa NMB ni koja ya huduma inayowaokoa na mikopo yenye masharti magumu zinazotolewa na watu mitaani.

“Huu mkopo wa NMB, unatusaidia sana na kutuepusha na kausha damu, kwani Mimi ambae napika hapa stendi siku nikiamka nimetumia hela yote kwa matumizi mengine nakopa hela huko nakwenda kununua mahitaji ya kupika na biashara inaendelea huku nikifanya marejesho” amesema Eva.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here