Home KITAIFA TRA YABORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUBORESHA UFANISI, UWAJIBIKAJI UKUANYAJI MAPATO

TRA YABORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUBORESHA UFANISI, UWAJIBIKAJI UKUANYAJI MAPATO

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya maboresho makubwa katika mifumo ya TEHAMA kwa lengo kuongeza ufanisi, uwajibikaji, uwazi pamoja na kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali. 

Miongoni mwa maeneo ambayo yamefanyiwa maboresho hayo ni katika stempu za Kodi za kieletroniki (ETS).

Kutokana na maboresho hayo yanayofanywa na TRA  hivi karibuni timu maalum ya ukaguzi iliyoongozwa na Meneja wa  ETS Ayubu Tweve iliitembelea Kampuni ya Double Diamond  Holdings Limited inayomilikiwa na Pardeep Singh Sindhu iliyopo  Njiro katika mkoa wa kikodi wa Arusha.

Kampuni hiyo  inayojihusisha na uzalishaji wa Pombe kali aina ya the The Ace of Diamond Gin na The Ace of Diamond Pineable na katika ukaguzi huo ilibainika kulikuwa na katoni 666 zikiwa zimebandikwa stamp zinazodhaniwa kuwa za kughushi pamoja na reel moja ya stamp inazodhaniwa kuwa ni ya kughushi.

Aidha timu maalum ya ukaguzi libaini pia  kulikuwa na katoni 995 zikiwa zimezalishwa muda mrefu lakini hazijabandikwa stamp  kinyume na utaratibu.Tayari mtuhumiwa amefikishwa katika vyombo vya usalama kwa hatua zaidi 

Akizungumzia maboresho hayo Meneja Mfumo  Eva Raphael amesema

 mfumo huo wa stempu za kielektroniki umeunganishwa na mifumo ya TRA ili kupata takwimu sahihi za uzalishaji/uagizwaji kwa maana ya idadi, ujazo pamoja na ubora na viwango vya bidhaa. 

Aidha TRA imewafahamisha wananchi wanaotumia bidhaa hizo kushiriki kulinda afya zao kwa kutambua bidhaa halisi na halali kwa matumizi yao.

Pia kutokana na wakusanya kodi kukabiliwa na changamoto ya kujua viwango vya kweli vya kodi kwa uzalishaji uliopo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifikiria kutafuta njia nyingine ya kisasa na sahihi ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Google search engine
Previous articleBenki ya NMB yaendelea kutoa elimu ya kifedha kwa wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam
Next articleWaziri Jenister Mhagama akoshwa na Mshikofasta ya NMB

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here