Home KITAIFA NAIBU WAZIRI MKUU ATETA NA WAFANYAKAZI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA

NAIBU WAZIRI MKUU ATETA NA WAFANYAKAZI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA

Google search engine

NA MWANDISHI WETU

-KAMPALA, UGANDA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko leo Oktoba 10, 2023 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda ili kupeana taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii yanayoendelea nchini.

Akitoa tathmini ya masuala mbalimbali ya kiuchumi, Naibu Waziri Mkuu amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anataka kuona nchi ikipiga hatua kiuchumi na kuwataka wafanyakazi kumsaidia kutimiza azma hiyo.

“Fanyeni kazi kwa uadilifu na Mheshimiwa Rais anathamini Sana mchango mnaoutoa kama ubalozi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kukuza uchumi,” amesema Dk. Biteko.

Akitoa tathmini juu ya masuala ya Nishati hususani Kuhusu masuala ya umeme, Dk. Biteko amesema miradi yote ya kimkakati iko kwenye hatua nzuri na kutolea mfano wa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere kuwa litaondoa  changamoto ya upungufu wa umeme na kuwezesha vituo vya kuzalisha umeme wa maji kufanya matengenezo na kuongeza pia kiwango cha gesi ili kufidia mapungufu yaliyopo

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi amewataka wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kuhakikisha wanatumia vema fursa za kibiashara zilizopo nchini Uganda kwa manufaa ya nchi yetu na kuongeza ushirikiano wa kibiashara na wadau wote.

Amesema, takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2022 uwekezaji kwenye masuala ya biashara ulikuwa karibu shilingi bilioni 138 kutoka Tanzania pekee na kuwa nchi ya tatu kwa uwekezaji nchini Uganda.

Kikao hicho kimedhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here