Home KITAIFA WAZIRI SILAA ATAKA USHIRIKIANO WIZARA YA ARDHI

WAZIRI SILAA ATAKA USHIRIKIANO WIZARA YA ARDHI

Google search engine
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akikabidhiwa ua na Katibu Muhtasi wa Wizara hiyo Joyce Mruma mara baada ya kuwasili ofisi za wizara hiyo eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 4 Septemba 2023.
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Ardhi alipowasili kwa mara ya kwanza eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 4 Septemba 2023.
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wizara na taasisi zake alipowasili kwa mara ya kwanza eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 4 Septemba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Na Rahma Sufiani, SJMC DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry William Silaa amewasili kwa mara ya kwanza ofisi za Wizara hiyo na kusisitiza ushirikiano pamoja na kuzingatia muda wakati wa utekelezaji majukumu ya wizara hiyo.

Silaa aliwasili ofisi za Wizara hiyo zilizopo eneo la Mtumba katika Mji wa Serikali jijini Dodoma tarehe 4 Septemba 2023 na kupokelewa na watumishi wa wizara hiyo wakiongozwa na Naibu Waziri Godfrey Pinda na Katibu Mkuu Mhandisi Antony Sanga.

“Napenda kuwashukuru sana namna mlivyonipokea katika siku yangu ya kwanza ninajisikia furaha kujumuika nanyi hivyo niwaombe tufanye kazi kwa ushirikiano ili kumsaidia Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan” alisema Silaa

Aidha, Waziri Silaa alikutana na Menejimenti ya utumishi ya Wizara ya Ardhi na kufanya kikao kifupi ambapo aliweka wazi vipaumbele vyake vikuu viwili na kuvitaja kuwa ni Ushirikiano na Muda.

“Mimi nina taratibu zangu za utendaji, kwanza kabisa ninaomba ushirikiano zaidi kazini kwani mimi nipo hapa kumsaidia Mh. Rais hivyo naomba muwajibike ili Rais akipita huko kwa wananchi wawe wanampigia makofi kumpongeza kutokana na utendaji mzuri tutaounesha,” amesema Waziri Silaa

“Nimefika mapema ofisini na nimeona baadhi wa watendaji wanakimbizana kwani wamekuja kwa kuchelewa ofisini sasa naomba tuongeze kasi zaidi ya kufika kazini, lakini pia naomba muwe huru kunishauri kwa lolote ili kuhakikisha tunafanya kazi kwa umoja na Ushirikiano,” amesema

Kwa mujibu wa Silaa utendaji kazi ndani ya Wzara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi unawezekana kutokana na ushirikiano, hivyo aliomba ushirikiano ili kumsaidia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.

Agosti 30, 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassani alifanya mabadiliko madogo katika safu ya baraza la mawaziri ambapo alimteua, Jerry William Silaa Mbunge wa jimbo la Ukonga kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akichukua nafasi ya Dk. Angeline Mabula mbunge wa jimbo la Ilemela.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here