Home KITAIFA NMB yasapoti Bonanza la Wabunge kwa milioni 130/=

NMB yasapoti Bonanza la Wabunge kwa milioni 130/=

Google search engine
Meneja wa NMB Kanda ya Kati ,Janeth Shango (wapili kulia) akimkabidhi jezi za michezo mbalimbali Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Festo Sanga (kushoto), makabidhiano hayo yalifanyika Bungeni Dodoma jana ,NMB ilikabidhi vifaa hivyo vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 130, kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Bunge ,Grace Matemu 

Mwandishi Wetu,Dodoma

BENKI ya NMB jana imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh milioni 90 kwa Timu ya Bunge huku wakisisitiza umuhimu wa mashirikiano.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni furana, traksuti na vifaa vingine vya michezo lakini NMB walikubali kutoa kifungua kinywa kwa wabunge wote na wageni pamoja na kuwawekea mahema kwaajili ya kukutumika katika bonanza hili ambapo ufadhili huo kwa ujumla wake unagharimu Sh130 milioni.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa mweneyekiti wa Bunge Bonanza Mheshimiwa Festo Sanga, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango alisema wanatoa vifaa hivyo katika muendelezo na utaratibu wao kwa taasisi za Serikali na wadau wengine kwani ndiyo utaratibu waliojiwekea.

Shango alisema utoaji wa vifaa hivyo siyo mara ya kwanza na haitakuwa mwisho kwani wanaendelea kuamini kuwa, Taifa bora ni lile linalojali afya za watu wake ikiwemo kwenye michezo. 

Meneja huyo wa kanda ya kati aliwaomba wabunge kuendeleza mashirikiano na benki hiyo kwa kuwa ni wadau ambao wanapaswa kufanya shughuli zao kwa pamoja kwani wote wanawahudumia wananchi.

“Lakini tuwaombe wabunge na wananchi kuendelea kuitumia benki yenu ya NMB kama ambavyo tumeendelea kuwa wamoja na sisi tunaahidi kuwa pamoja nanyi kwa kila jambo ili mradi tujenge nchi yetu kwa kuwa na watu wenye afya njema,” alisema Shango.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Bonanza la Bunge Fessto Sanga alisema msaada huo kutoka NMB siyo mara ya kwanza kwani hata kwa mwaka huu imekuwa ni mara ya pili wakiwafadhiri.

Alisema katika bonanza la kwanza walipokea vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni jambo linalofanya kwa mwaka huu pekee kuwa wamepata ufadhiri wa zaidi ya Sh230 milioni kutoka benki hiyo.

Sanga alisema vifaa vilivyotolewa na NMB vinawasaidia kwenye mabonanza yao ikiwemo michezo itakayofanyika (Septemba 2,2023) ambalo ni maalumu kwa mashindano ya wabunge na watumishi wa ofisi ya bunge.

Kwa upande wa wabunge watashirikiana na wenzao wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na michezo itaanzia Chuo cha Mipango Dodoma kuelekea Viwanja vya Jonmerini.

Mbunge huyo wa Makete alisema mgeni rasmi katika bonaza hilo lenye lengo la kupambana na magonjwa yasiyo na kuambukiza atakuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zuber Ali Maulid.

Mwenyekiti huyo alitaja michezo itakayokuwepo katika bonanza hilo ni Mpira wa miguu,pete,bao,kukimbia,mwendokasi,kupita kwenye pipa na mingine.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here