Home MICHEZO TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI AFCON 2023, YAIFUNGA NIGER 1-0

TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI AFCON 2023, YAIFUNGA NIGER 1-0

Google search engine

Na Eleuteri Mangi, WUSM Dar es Salaam

Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imeicharaza timu ya Niger goli 1-0 na kufufua matumaini ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 nchini Ivory Coast.

Saimon Msuva mfungaji wa goli hilo ndiye shujaa wa mchezo huo uliochezwa Juni 18, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewaongoza watanzania kuishangilia timu yao akiwa Mgeni Rasmi katika mchezo huo hatua iliyoongeza hamasa.

Mchezo huo umeshuhudiwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu wake Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Wales Karia.

Tanzania ipo kundi F pamoja na timu za mataifa ya Algeria, Niger na Uganda kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here