Home MICHEZO MICHUANO YA DK. SAMIA CUP YAZINDULIWA WILAYANI SAME

MICHUANO YA DK. SAMIA CUP YAZINDULIWA WILAYANI SAME

Google search engine
Wachezaji wakipepetana kuwania mpira
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kaslida Mgeni, akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya Dk. Samia Cup
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kaslida Mgeni akipeana mikono na wachezaji wakati wa uzinduzi wa Samia Cup
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Mussa Mwakitinya akizungumza wakazti wa uzinduzi wa michuano ya Samia Cup wilayani Same

Na ASHRACK MIRAJI

-SAME, KILIMANJARO 

MKUU wa Wilaya ya Same, Kaslida Mgeni amewaasa vijana kuacha tamaa kuiga tamaduni zisizo faa zilizo kinyume na maadili yaliyo kwenye jamii ikiwemo mcheo mchafu wa kujihusisha katika mapenzi ya jinsia moja, biashara haramu ya Dawa za Kulevya Kilimo cha Bangi na Mirungi miongoni mwa viashiria vinavyo tajwa kuathiri vijana kuwa katika hatari ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya Dk. Samia CUP, mashindano yaliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango akisema uamuzi huo wa mbunge kuanzisha mashindano utasaidia kuibua vipaji hasa kwa vijana washiriki, pia kuimarisha afya kama inavyo sisitizwa na serikali miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na magonjwa nyemelezi.

“Kipekee nimshukuru sana mbunge sote tunaona kazi kubwa anayoifanya kupambania wananchi kwenye jimbo lake hususani katika kuleta maendeleo hivyo niendelee kutoa rahi  kwa vijana kushiriki kikamilifu kwenye michezo hii.

“… kwakua itasaidia kupunguza muda wa kukaa vijiweni bila shughuli maalum ambako ndiko mnakutana na vishawishi na kujiingiza kwenye michezo isiyofaa,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Akifungua michezo hiyo Naibu katibu mkuu Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) , Mussa Mwakatinya, amesema Dk. Samia Cup imekuja ikiwa ni namna ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa iliyofanyika kwenye Jimbo la Same Mashariki ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Barabara, ujenzi wa madarasa kwenye Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari pia uboreshwaji wa huduma za afya, michezo hiyo inalenga pia kukuza vipaji na kujipatia ajira na kuimarisha afya kuwezesha kuendelea kuchapa kazi.

“Michezo huondoa mawazo potofu kwa vijana kama wizi na ubakaji kwa mabindi zetu hivyo kama wananchi wa Jimbo la Same Mashariki na vijana kwa ujumla tumuunge mkono Mbunge kwani anafanya kazi kubwa kwa maslahi ya jimbo lake na kama mnavyo jionea kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuboresha huduma, jukumu kubwa la mbunge ni kuweka msukumo kuikumbusha Serikali kwenye usimamizi wa ilani,” amesema

Kwa upande wake katibu wa Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, amesema dhumuni la kuanzishwa kwa mashindano hayo ni kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa shughuli mbalimbali zilizofanyika kwenye jimbo hilo ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali hasa ujenzi wa vituo vya afya, ukarabati wa Barabara pamoja na uboreshwaji wa miundombinu kwenye Shule za Msingi na Sekondari.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here