Home BIASHARA NMB yawapiga msasa Wanawake wa TUICO Morogoro

NMB yawapiga msasa Wanawake wa TUICO Morogoro

Google search engine
Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu wa Benki ya NMB,Joanitha Mrengo akizungumza na kusalimiana na washiriki wa Semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wanawake wanachama wa TUICO Mkoa wa Morogoro kutoka Sekta isiyo rasmi wa jamii ya Kimasai

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO 

WANAWAKE wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri Tanzania (TUICO), wametakiwa kuvutiwa na mafanikio kitaifa na kimataifa ya Hati Fungani ya Jasiri ya Benki ya NMB ‘NMB Jasiri Bond,’ na kuyatumia kama chachu ya kuendelea kuwa wateja waaminifu wa benki hiyo ili kuwa sehemu ya mnyororo wa wanufaika wa huduma zenye lengo la kusaidia ustawi wao kimaisha na kukua kiuchumi. 

Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu wa Benki ya NMB,Joanitha Mrengo (kulia) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu TUICO, Takim Salehe (kushoto) pamoja na mkurugenzi wa mashirika ya fedha TUICO, Peles Jonathan Hageze (katikati) baada ya kufungua Semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wanawake wanachama wa TUICO Mkoa wa Morogoro.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Joanitha Mrengo, alipomwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, katika Semina ya Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi Wanawake ambao ni Wanachama wa TUICO Mkoa wa Morogoro, iliyofanyika kwa siku moja, ikihudhuriwa pia na viongozi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Shirika la Kazi Duniani (ILO), na kudhaminiwa na benki hiyo.

Aprili mwaka jana, NMB ilihitimisha mauzo ya Hati Fungani ya Jasiri kwa kuvuna kiasi cha Sh. Bil. 74 na kuvuka lengo la kukusanya Sh. Bil. 25 pesa zilizotumika kutanua wigo wa utoaji huduma za mikopo kwa kampuni zinazoendeshwa na wanawake, ama kampuni zinazozalisha bidhaa zinazowagusa wanawake nchini.

Ni mafanikio yaliyoipa NMB tuzo mbalimbali, zikiwemo za Hati Fungani Bora ya Mwaka iliyotolewa na Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Jukwaa la Ufadhili wa Ujasiriamali (SME’s Finance Forum), pamoja na Tuzo ya Platinum ya Kundi la Dhamana Endelevu iliyotolewa nchini Cambodia, kote ikitambulika kama hati fungani wezeshi kwa wanawake, kiasi cha kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Luxemburg (LuxSE), ambalo ni moja ya masoko makubwa ya hisa duniani.

Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu wa Benki ya NMB,Joanitha Mrengo akizungumza na kusalimiana na washiriki wa Semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wanawake wanachama wa TUICO Mkoa wa Morogoro

Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mrengo alisema mafanikio hayo, pamoja na kutambuliwa kwa benki yake kuwa miongoni mwa taasisi kinara katika mgawanyo wa kiuchumi kwenye suala la kijinsia (EDGE Certificate), ambako NMB ni taasisi ya kwanza Afrika kutunukiwa cheti, vinapaswa kutazamwa kwa jicho la ziada na wanawake wote nchini, wanaopambania ukuaji wao kiuchumi. 

“Wafanyakazi wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kazi, ikiwa ni pamoja na kutafuta Usawa wa Kijinsia, kujaribu kufikia malengo yao ya kazi na kuboresha Ustawi wa Jamii. Hivyo NMB tunaamini semina hii itawajengea uwezo katika nyanja za uongozi na uchumi.

“Sisi NMB tunatambua na kuthamini umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uwezo wa wanawake katika jamii yetu, kwani tunajua wanaweza kuchangia ukuaji wao kiuchumi na ustawi wa jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla, ndio maana tukatenga fungu kubwa la fedha za mikopo na huduma mbalimbali za kifedha kwa wanawake wajasiriamali na wafanyakazi,” alisisitiza Mermaid katika semina hiyo.

Naye Naibu Katibu  Mkuu wa TUICO, Tamim Salehe, aliishukuru NMB kwa kushirikiana na chama chake katika kuwanoa wanawake wanachama wa mkoa wa Morogoro, huku akiwataka washiriki wote kuitumia vema semina hiyo sio tu kwa kuzingatia maelekezo, bali pia kujenga mtandao wa kiushirikiano baina yao ili kusaidiana maarifa ya utatuzi wa changamoto mahali pa kazi ama biashara zao. 

Tamim alizishukuru ATE, ILO, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na taasisi nyingine kwa kushiriki na kufanikisha semina hiyo, ambayo pia ilitumika kuwaelimisha wanawake juu ya uongozi katika chama, jamii na taasisi za  kazi, kuwaongezea uelewa wa agenda ya Usawa wa Kijinsia (50 kwa 50), kushirikisha wanawake katika shughuli na mipango ya TUICO – chama kinachojumuisha wadau wa sekta nne za Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha na Huduma na Ushauri. 

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here