Home KITAIFA Rais Samia arudisha shangwe nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi nchini

Rais Samia arudisha shangwe nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi nchini

Google search engine

Rais Samia Suluhu Hassan akipunga mkono kwenye sherehe za Mei Mosi mjini Morogoro

Rais Samia arudisha shangwe nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi

Na Mwandishi Wetu

-BEST MEDIA, MOROGORO

MATUMAINI mapya sasa yameibuka kwa wafanyakazi nchini. Ndivyo unavyoweza kusema, hasa baada ya Mkuu wa nchi Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kurejeshwa kwa utaratibu wa nyongeza ya ya mishahara kwa wafanyakazi wa umma nchini.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa … “Wafanyakazi mambo ni moto… Mambo ni fire,’ ambapo ni kauli ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akitangaza kurejesha nyongeza ya mishahara ya kila mwaka kwa wafanyakazi wa umma ikiwa ni miaka saba tangu kuondolewa kwa mfumo huo na Rais wa Awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli mwaka 2016.

Kutokana na hali hiyo, Samia amewasihi wafanyabiashara kutoongeza bei madukani huku akiwaahidi wafanyakazi kuwa mambo mazuri yanakuja pasipo kutangaza hadharani nyongeza hiyo.

Hata hivyo Mei 14, 2022  Rais Samia aliridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, ambapo Sh trilioni 1.59 ilitumika kwa ongezeko hilo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Katika hotuba yake leo Jumatatu Mei Mosi, 2023 wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) kitaifa yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro Rais Samia ametoa ufafanuzi wa nyongeza hiyo.

“Mishahara kwa mwaka huu mbali na upandishaji wa posho nilizosema tumejiandaa pia kupandisha madaraja, vyeo vitaendelea kupandishwa, kutenganisha makundi na madaraja mserereko wale ambao hawakupata mwaka jana watapata mwaka huu.

“Niseme pia kuna nyongeza za mishahara za mwaka ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zimesitishwa, nikaona kwa mwaka huu tuzirudishe kwa wafanyakazi wote kuna nyongeza za mishahara tunaanda na tutaendelea kama tulivyokuwa tunafanya zamani,” amesisitiza.

Havyo Mkuu huyo wa nchi amesisitiza kuwa mwaka jana Serikali ilipandisha mishahara kwa asilimia 23.3 ambayo si kila mtu alifaidika ila lengo ilikuwa kuwainua wa kima cha chini na wengine wachache lakini kuna kindi kubwa halikuguswa.

“Nikiwemo mimi mfanyakazi namba moja. Lakini kingine tulipandisha posho za wafanyakazi na waliofaidika kwenye hili ni wafanyakazi wenye mishahara mikubwa ambao hawakufaidika na ile nyongeza za mishahara ya asilimia 23.3, nafahamu kuna baadhi ya taasisi hawakuweza kulipa tulipotoa posho tayari bajeti zilishapita kwa maana hiyo mavuno yatakuja mwaka huu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono viongozi pamoja na Wafanyakazi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.
Wafanyakazi kutoka Wizara, Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kutoa ujumbe kuhusiana na masuala mbalimbali ya Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here