Home KITAIFA HATUA MUHIMU KUMALIZA MIGONGANO YA BINADAMU, WANYAMAPORI ZATAJWA

HATUA MUHIMU KUMALIZA MIGONGANO YA BINADAMU, WANYAMAPORI ZATAJWA

Google search engine
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Fortunata Msofe (kushoto), Afisa Wanyamapori Mkuu na Mratibu wa Maliasili, Mazingira na Mabadiliko ya tabianchi kutoka ofisi ya Rais-TAMISEMI, Hawa Mwechaga (katikati) na Mkuu wa Utafiti kutoka TAWIRI, Dkt. Stephen Nindi (kulia).

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

HATUA ya kuibuka kwa migongano baina ya binadamu na wanyamapori imetejwa kama changamoto hasa kwa wananchi kuhisi wanaonewa, sasa njia za kumaliza tatizo hio umetajwa.

Hilo limekuja wakati ikiwa inaripotiwa kwa nyakati mbalimbali juu ya uwapo wa tembo kwenye makazi ya watu ambapo hilo linatajwa kumalizika kwa suala hilo nikwa mamlaka za Serikali kupanga matumizi bora ya Ardhi ikiwamo kuheshimu shoriba za wanyamapori.

Kutokana na kibuka kila mara kwa taarifa za aina hiyo, jambo lililoifanya Serikali ya Tanzania kutekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yaliyopakana na hifadhi na ukanda wa Ruvuma ni miongoni mwa maeneo yaliyofikiwa na mpango huo.

Lengo kuu la mpango huo ni kuondoa kabisa migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori, ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ni tatizo kwa baadhi ya maeneo kwenye ukanda huo wa Ruvuma.

Afisa Mtafiti Mkuu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Stephen Nindi akitoa maelezo ya namna serikali ilivyoshiriki katika kukabiliana na Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori katika ukanda wa Ruvuma.

Akizungumza Juni 6, 2024 jijini Dar es Salaam, wakati wa mdahalo wa asubuhi ulioandaliwa na  Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa Mradi wa Kupunguza Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania, unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani (BMZ),  Afisa Mtafiti Mkuu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Stephen Nindi ameweka wazi kuwa mpango wa matumizi ora ya ardhi utasaidia kuondoa migongano hiyo.

Katika mdahalo huo ambao pia uliwapa nafasi wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuileza jamii kile ambacho serikali kwa kushirikiana na wadau wake wamefanikiwa kukifanya katika kukabiliana na migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori kwenye ukanda wa Ruvuma.

Dkt. Nindi alisema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika kukabiliana na migongano hiyo na miongoni mwao ni kutekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi.

“Ikitokea maeneo yote yakawekwa kwenye mpango wa matumizi bora ya Ardhi, hii migongano baina ya Binadamu na Wanyama itapungua ama kwisha kabisa.

“Shoroba za wanyamapori , maeneo ya uvuvi wa mabwawa, sehemu za kulishia mifugo na maeneo ya kilimo yote yatatengwa kwa utaratibu utakaokuwa na faida kwa pande zote.

“Serikali imeshaanza kulifanya hilo na mpango wa matumizi bora ya ardhi umeanzia ngazi ya taifa na umeshuka mpaka kwenye ngazi ya wilaya, hii inatoa nafasi kwa wadau wengi zaidi kushriki katika kuutekeleza mpango huu, maana mpango uliopo ngazi ya chini unakuwa umebeba taarifa nyingi zaidi ambazo zinarahisisha utekelezaji wake,” alisema Dkt. Nindi

Alisema kama tembo na wanyamapori wengine wakitengewa njia zao, haitakuwa rahisi kwao kuingia kwenye maeneo ya binadamu iwe ya mashamba au makazi, kama ambavyo binadamu wakizijua shoroba za wanyamapori hawataweza kuziharibu kwa kufanya shughuli zao humo.

Mdahalo huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Kupunguza Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani (BMZ).

Kwa upande wake Meneja Mtekelezaji wa Mradi huo kutoka GIZ, Christina Georgii, alisema wanafurahia kutekeleza mradi huo, ambapo ameahidi shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

“Tunafurahia kutekeleza mradi huu wa Kupunguza Migongano Baina ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania, tunaamini hatua hii itasaidia kufanya binadamu kuishi kwa amani na wanyamapori, GIZ tutaendelea kushirikiana na serikali na wadau wetu kama tunavyofanya kwa JET,” alisema Christina

Kimsingi ongezeko la shughuli za kibidamu hasa kilimo na ufugaji vinatajwa kuwa chanzo kikuu cha migongano baina ya binadamu na wanyamapori na kwamba suala hilo limekuwa ni changamoto kwenye baadhi ya maeneo nchini.

Takwimu za TAWA za wanyamapori kuingia kwenye makazi na mashamba ya binadamu kwa mwaka 2016/17 zinaonesha kuwa kulikuwa na matukio 833 na mwaka 2027/18 kulikuwa na ongezeko la matukio 164 huku mwaka 2018/19 yalifikia matukio 1510, mwaka 2019/20 matukio hayo yalipungua kutoka 1510 hadi 1426.

Kupungua huko kulichangiwa na uzuri wa hali ya hewa iliyochangia kupatikana kwa malisho ya kutosha kwenye maeneo yao.

Hata hivyo mwaka 2020/21 hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi kwani matukio 1706 yaliripotiwa na kuanzia hapo hali iliendelea kuwa mbaya zaidi kwani mwaka 2021/22 yaliripotiwa matukio 2304 na mwaka 2022/23 yalifikia matukio 2817.

Alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 23.76 kwa mwaka na uharibifu wa mazao ukiwa ni ongezeko la wastani wa asilimia 118..1 kwa mwaka. 

Kwa mujibu wa takwimu hizo za TAWA, ni wazi mwaka 2018 kulikuwa na ongezeko kubwa la matukio ya migongano, ongezeko liliifanya Wizara ya Maliasili na Utalii kuandaa Mkakati wa Taifa wa kusimamia migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori wa mwaka 2020-2024.

Mkakati huo ulizinduliwa Oktoba 5, 2020 na hadi sasa unatekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa -TANAPA, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro -NCAA, TAWA, Wakala wa Misitu Tanzania -TFS, TAWIRI  na wadau wengine wa masuala ya uhifadhi.

Tatizo hilo unazigusa wilaya 44 ambazo zinakabiliwa na changamoto ya wanyamapori kurejea kwenye njia zao za awali hatua inayoonekana ni kama wanavamia maeneo ya watu na kusababisha uharibifu wa mazao, kujeruhi na wakati mwengine kusababisha vifo kwa binadamu.

Hatua hiyo haiwaathiri binadamu pekee, kwani hata wanyama nao wanaathirika kwa kujeruhiwa na wakati mwengine kuuawa na binadamu.

Busega, Kilosa, Meatu, Nachingwea, Rufiji, Lindi, Manyoni, Itilima, Tunduru na Bunda ndiyo maeneo yanayotajwa kuwa na tatizo hilo huku tembo akitajwa kuongoza kwa asilimia 80 kuwa na matukio ya kurejea kwenye njia zake na kuingia kwenye makazi ya watu, simba, fisi na nyani wanabeba asilimia 20 ya matukio yote.

HEWA UKAA

Kutokana na hali hiyo jamii imetakiwa kutambua fursa inayopatikana katika biashara ya hewa ukaa kiwa njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mratibu wa Maliasili, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Hawa Mwechaga, alliwataka Watanzania kuangalia fursa hizo na kuona suala la hilo tabianchi si adhabu.

Mwechaga, alisema kuwa ipo haja ya jamii kuelemishwa juu ya fursa zinazopatikana katikati ya tatizo la mabadiliko ya tabia nchi, ambapo pamoja na kujiingizia kipato lakini pia mtu anashiriki moja moja kutunza misitu, hatua inayoepusha kasi ya ongezeko la tatizo hilo.

Mratibu huyo alisema yapo baadhi ya maeneo yameanza kunufaika na biashara ya Hewa Ukaa na Serikali imekuwa mdau mkubwa wa kuhakikisha biashara hiyo inafanyika katika maeneo mengi yenye misitu ya asili.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here