Home KITAIFA MKURUGENZI TMDA: HAKUNA DAWA ZA KUONGEZA MAKALIO, MATITI WALA VIUNGO KWA BINADAMU

MKURUGENZI TMDA: HAKUNA DAWA ZA KUONGEZA MAKALIO, MATITI WALA VIUNGO KWA BINADAMU

Google search engine
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dk. Adam Fimbo akizungumza na wahariri katika kikao kazi kilichofanyika leo Mei 16, 2024, mjini Iringa

Na MWANDISHI WETU

-IRINGA

HATIMAYE Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imevunja ukimya na kusema kuwa hadi sasa hakuna dawa ya kuongeza makali, matiti na viungo vingine kwa binadamu.

Kutokana na hali huyo imesema kuwa mabadiliko ya mwili wa binadamu kama anatahiaji kufanya hivyo anaweza kuyapata kwa upasuaji lakini si kwa dawa.

Akizungumza leo Mei 16, 2024 mjini Iringa, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dk. Adam Fimbo, amesema kuwa ni lazima jamii ikubali kutopotoshwa na matangazo yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii.

Dkt. Adam Fimbo, amesema pamoja na jitihada za mamlaka hiyo katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu shughuli za udhibiti wanazofanya, bado uelewa uko chini kitu kinachoathiri utendaji wa mamlaka hiyo.

Kutokana na hali hiyo licha ya kuwepo kwa upotoshaji kwa jamii ni lazima ijue kwamba hakuna dawa za kuongeza makalio wala kukuza viungo kwa binadamu.

“Ninachotaka hapa kwamba zipo dawa za kupunguza unene ila sisi ndani ya TMDA hatuna dawa yoyote tuliyoletewa na tukaifanyika uchunguzi ya kukuza makalio, matiti  wala kukuza viungo kwa binadamu na nyingi zinazokuja kwenye ni lishe za kawaida tu. Na ukitaka labda kufanya hayo ili kuona mabadilio labda ufanye upasuaji

“Kiwango hiki cha uelewa kinasababisha matumizi yasiyo sahihi ya Dawa, idadi ndogo ya wananchi wanaripoti maudhui ya Dawa na baadhi ya wafanyabiasha kuingiza Dawa duni na bandia pamoja na wananchi kutozingatia tarehe ya kuisha matumizi ya bidhaa,” amesema Dkt. Fimbo.

Aidha amesema alisema hali hiyo inapelekea mamlaka kuendelea kutumia mbinu mbalimbali kuelimiaha jamii.

“Mamlaka inatambua mchango wa vyombo vya Habari katika kuongeza ulewa wa wananchi kuhusu shughuli za Udhibiti zinazofanywa na Mamlaka na kwamba uelewa mzuri wa waandishi na Wahariri wa vyombo vya Habari ni msingi wa uelimishaji jamii,” amesema Dkt. Fimbo.

Katika kika kikao kazi hicho mada saba zilitolewa ikiwemo Udhibiti wa bidhaa, Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Sura 219, Bidhaa bandia na Udhibiti wake na ufuatiliaji na utoaji taarifa kwa madhara yatokanayo na bidhaa.

Mada nyingine ni zilizotolewa kwe kikao hicho ni Huduma za Maabara ya TMDA, uzoefu wa Udhibiti katika Kanda ya kati na mchango wa vyombo vya Habari katika Udhibiti.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here