Home KITAIFA MCHENGERWA ALIOMBA BUNGE BAJETI YA TRILIONI 10.125/- TAMISEMI

MCHENGERWA ALIOMBA BUNGE BAJETI YA TRILIONI 10.125/- TAMISEMI

Google search engine

*UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI KUTAFUTA BILIONI 17.70

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

OFISI ya Rais – TAMISEMI, imeomba Bunge kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2024/25 yenye jumla ya Sh trilioni 10.125 ikiwa ni ongezeko la karibu trilioni moja ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2023/24.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Mchengerwa ameliambia Bunge kuwa mwaka 2023/24, Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliidhinishiwa bajeti ya Sh trilioni 9.18, kati ya fedha hizo, trilioni 3.52 ni fedha za maendeleo na trilioni 5.65 ni za matumizi ya kawaida.

Hadi kufika Machi, 2024 ofisi ilikuwa imekusanya na kupokea Sh trilioni 6.99 sawa na asilimia 76.18 ya fedha zilizoidhinishwa na kati ya hizi trilioni 4.47 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh trilioni 2.52 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikijumuisha Sh trilioni 2.06 fedha za ndani na Sh bilioni 456.39 fedha za nje.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara, sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa na taasisi zake kwa mwaka 2024/25, Mchengerwa amesema kati ya fedha zinazoombwa, zaidi ya Sh trilioni 6.71 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida wakati zaidi ya Sh trilioni 3.42 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo zaidi ya Sh trilioni 2.27 ni fedha za ndani na Sh trilioni 1.145 ni fedha za nje.

Mchengerwa amesema katika mwaka 2024/25, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, taasisi zilizo chini yake, mikoa 26 ikijumuisha halmashauri 184 imepanga kukusanya maduhuli na mapato ya ndani jumla ya zaidi ya trilioni 1.60 ikilinganishwa na Sh trilioni 1.14 iliyoidhinishwa mwaka 2023/24, ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 456.89 sawa na asilimia 39.93.

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Waziri huyo wa TAMISEMI, alisema kuwa katika mwaka 2024/25 Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetenga shilingi bilioni 17.79 kwa ajili ya kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024.

Alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 8.00 ni fedha kutoka Serikali kuu kwa ajili ya uratibu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Makao Makuu)na Shilingi bilioni 9.79 ni mchango wa halmashauri kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kugharamia uchaguzi huo. Uchaguzi huu utahusu uchaguzi wa viongozi katika ngazi ya msingi ambao ni wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji, wajumbe wa halmashauri ya vijiji na wajumbe wa kamati za mitaa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here