Home KITAIFA RAIS DK. HUSSEIN MWINYI ASHUKURU KWA DUA NA KHITMA ZA HAYATI MZEE...

RAIS DK. HUSSEIN MWINYI ASHUKURU KWA DUA NA KHITMA ZA HAYATI MZEE MWINYI

Google search engine
RAais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi

Na MWANDISHI WETU

-ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru kwa niaba ya familia Waumini wa Dini ya Kiislamu sehemu mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar walioandaa Dua na Khitma ya kumwombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo katika Khitma na Dua Maalum ya kumwombea Baba yake mzazi , Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi iliyoandaliwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar katika Masjid Mushawar Mwembe Shauri Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Machi 11, 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi pia amewashukuru wananchi wote walioshiriki katika Dua hizo, ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa wa Serikali, Dini na Vyama vya Siasa wameshiriki Dua na Khitma hiyo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here