Home KITAIFA NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AWASILI RASMI OFISINI

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AWASILI RASMI OFISINI

Google search engine

*Apokewa na Katibu Mkuu na wafanyakazi wa wizara, aahidi kushirikiana na wadau kumsaidia Rais Samia kufikia malengo

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio (kulia)
akipokea maua mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi za Wizara ya
Nishati, Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma leo Machi 11, 2024.

Na MWNDISHI WETU

-DODOMA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio  amewasili rasmi ofisini na kuahidi kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.

Alipowasili Ofisi za Wizara eneo la Mtumba, jijini Dodoma alipokewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo, Mhandisi Felchesmi Mramba,  Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Nishati.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto)
akimkaribisha katika Ofisi za Wizara ya Nishati Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio mara baada ya kuwasili rasmi
katika Ofisi za Wizara, Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya mapokezi, Dk. Mataragio amesema, ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kuyafikia matarajio ya viongozi na Taifa kwa ujumla.

“Mimi nashukuru kwa kuteuliwa kutumika katika nafasi hii, na nitaendeleza ushirikiano  na watumishi wenzangu, ili kumsaidia Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake,” amesema Dk. Mataragio.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here