Home BIASHARA NMB YATOA MIZINGA 500 YA KISASA YA UFUGAJI NYUKI MIKOA MITATU

NMB YATOA MIZINGA 500 YA KISASA YA UFUGAJI NYUKI MIKOA MITATU

Google search engine
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbas (wa pili kulia), akipokea sehemu ya mizinga 200 ya kufugia nyuki kwa ajili ya vikundi vya ufugaji vya wilaya za Gairo na Kilombero, kutoka kwa Afisa Mkuu wa Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shao, wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa Programu ya ugawaji mizinga hiyo kwa wafugaji wa mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe. Uzinduzi huo ulifanyika katika msitu wa Msingisi uliopo eneo la Kijiji cha Msingisi, wilayani Gairo. Wa pili kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango na kulia Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabir Makame. Na Mpiga Picha Wetu. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbas wa pili kutoka kulia akipokea mmoja wa mzinga wa nyuki kutoka kwa Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali Benki ya NMB, Alfred Shao kutoa  mizinga 500 ya kisasa ya ufugaji nyuki kwa vikundi 17 vya ufugaji nyuki katika mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe wakati wa ufunguzi wa kitaifa wa ugawanyi wa mizinga ya nyuki wilaya ya Gairo mkoani Morogoro na kutoka kushoto ni Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kati, Janeth Shango na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Gairo, Jabir Makame.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbas (kulia), akimkabidhi moja kati ya mizinga ya nyuki iliyotolewa na Benki ya NMB kwa mwakilishi wa kikundi cha Juhudi Msingisi, Naomi Mbuhe, wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa Programu ya ugawaji mizinga hiyo kwa wafugaji wa mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe. Uzinduzi huo ulifanyika katika msitu wa Msingisi uliopo eneo la Kijiji cha Msingisi, wilayani Gairo. Wa pili kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shao. Na Mpiga Picha Wetu. 

Na MWANDISHI WETU

-MOROGORO

SERIKALI imesema Tanzania ina mazingira mazuri ya uzalishaji wa mazao ya nyuki yenye kiwango cha juu cha ubora kutokana na uwepo wa misitu yenye mimea inayotoa chakula kwa nyuki huku sekta hiyo ikichangia ajira zaidi ya ajira ya watu milioni mbili na kukadiliwa kuwa na uwezo wa uzalishaji wa asali tani 138,000 kwa mwaka.

Akizungumza katika uzinduzi wa kitaifa wa ugawaji wa mizinga 500 iliyotolewa na benki ya NMB wilayani Gairo mkoani hapa, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbas amesema uzalishaji watani 138,000 za asali ya nyuki kwa mwaka ni kiwango kidogo ikilinganishwa na fursa zilizopo na tathmini iliyofanywa na wizara hiyo inaonesha kuwa asilimia 90 ya wafugaji nyuki nchini wanatumia mizinga ya jadi.

Dk. Abbas amesema mizinga hiyo ya jadi inachangia uharibifu wa misitu kwani utengenezaji wake unahusisha ukataji wa miti hivyo wadau na serikali wanajukumu la kuendeleza sekta hiyo kwa kuandaa mazingira mazuri ya upatikanaji wa mizinga ya kisasa ambayo italeta tija na kulinda misitu.

“Mizinga ya jadi inazalisha kiwango kidogo cha asali lakini asali ya Tanzania inakubalika kwenye masoko mbalimbali nje ya nchi sekta za misitu na ufugaji nyuki zinachangia wastani wa asilimia 3.5 ya pato ghafi la taifa ukilinganisha na fursa za rasilimali za misitu na nyuki zilizopo na niwaombe wenzetu wa NMB kuongeza mizinga ya kisasa ifikie 600 wakati serikali ikiandaa na kutekeleza mikakati ya ujenzi wa viwanda ambavyo kwa sasa vipo sana vya kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki,”amesema Dk. Abbas.

Juhudi hizi pia ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani utakaofanyika Tanzania mwaka 2027, ambao utawahusisha waataalum wakimataifa  zaidi ya 4000.

Kwakweli Benki ya NMB mnastahili pongezi kubwa sana kwa kuzindua Programu Endelevu ya Ugawaji Mizinga ya Nyuki 500 kwa vikundi 17 vyenye wafugaji zaidi ya 300, katika mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe, mkishirikiana na Mamlaka ya Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFS).

Afisa Mkuu wa wateja wakubwa na serikali benki ya NMB, Alfred Shao amesema benki hiyo imewezesha kutengeneza mizinga 500 ya kisasa kwa ajili ya kuwagawia wafugaji nyuki katika mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe.

Shao amesema licha ya kutoa mizinga hiyo, benki hiyo imetenga sh41milioni kwa ajili ya kuwezesha mafunzo kwa wanufaika wa mizinga hiyo katika mradi wa kusapoti ufugaji wa nyuki.

“Nyuki ili wazaliane ni lazima misitu ilindwe na moja ya sababu ya NMB kutoa mizinga hii 500 ni juhudi za kulinda misitu yetu ikienda sambamba na upandaji miti ambapo mpaka sasa miti 750,000 tayari imepandwa nchini kwa kushirikiana na TFS na wananchi wanapata mazao ya misitu kwa kutunza mazingira.”amesema Shao.

Shao amesema Benki ya NMB kupitia NMB Foundation imetoa mizinga 500 ya kisasa kwa mikoa mitatu ambapo mkoa wa Morogoro umepata mizinga 200, Tabora 200 na Njombe 100 kwa vikundi 17 vya ufugaji nyuki na vikundi hivyo vitapatiwa elimu ya ufugaji nyuki wa kisasa, elimu ya kifedha na elimu ya uvunaji wa asali ili asali itayovunwa iwe ya ubora wa kiwango cha juu na kuuzwa nje ya nchi.

“Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeweka mkazo mkubwa katika sekta ya asali na nyuki, ambako tayari kuna Watanzania takribani milioni mbili wamejiari huko, na tunatambua hii ni sekta ya kimkakati ambayo ikitiliwa mkazo, itawakwamua wengi, vijana tuipe mkazo sekta hiyo ambayo ni itakuwa ya kijanja zaidi huko tuendako, yenye ‘maokoto’ ya kutosha,”ameongeza Dk. Abbas.

“Usisubiri NMB waje, anza leo wakukute pazuri. Sekta hii inachangia Pato la Taifa kwa asilimia 3.5, pia mazao ya misitu na asali yanachangia asilimia 5.9 ya fedha za kigeni, huasusani Dola za Kimarekani, sio sekta yenye eneo dogo, bali ina mawanda mapana, vijana wasidharau sekta zenye kuingiza pesa kama hii, ambayo Serikali hatulali kwa kuchakata mipango mikubwa juu yake.

“Tumeanza ujenzi wa viwanda saba vya kuchakata na kufungasha asali, ili kukuza uchumi ambako Serikali imewekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 katika mikoa ya Tabora, Katavi, Geita, na Kigoma, NMB mtapoenda huko mtawakuta wafugaji. Mradi mwingine ni wa Sh. Bilioni 27 wa kujenga madarasa na mabweni ya Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora, NMB tunawaomba mje kuona uwekezaji wetu,” alibainisha.

Dk. Abbas aliongeza ya kwamba, Rais Samia hivi karibuni amefanya uamuzi mgumu wa kimkakati, kwa kuiingiza sekta ya asali na nyuki katika Programu ya Kujenga Kesho Iliyo Bora kwa Vijana na Wanawake nchini (BBT), hivyo akaziomba Sekta za Fedha na Sekta Binafsi, zifuate nyayo za NMB kwa kuisapoti Serikali katika kuipa thamani zaidi Kampeni ya Achia Shoka, Kamata Mzinga.

“Tutawaalika wadau tutapokamilisha kampeni hiyo waone jinsi ya kusaidiana na Serikali, ili kutanua sekta hii kuelekea Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani hapo mwaka 2027, utakaowaleta nchini zaidi ya washiriki 4,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani. Mkutano huo ni uthibitisho wa Jumuiya ya Kimataifa kuridhishwa na hatua iliyopigwa na Serikali ya Rais Samia,” amesisitiza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Gairo, Jabir Makame amesema programu ya boresha mazingira na uchumi kupitia ugawaji wa mizinga kitaifa kufanyika wilaya ya Gairo na wataendelea kuwapa hamasa jamii ya wilaya hiyo kuendelea kuhifadhi na kutunza mazingira.

Kamishna wa Uhifadi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) TFS, Profesa Dos Santos Silayo amesema benki ya NMB imekuwa na ushirikiano nao katika utunzaji mazingira na upandaji miti tangu mwaka 2022 na sekta ya ufugaji nyuki inaonekana kama ni kazi ya wazee na kuwekeza nguvu utawafanya riba nyingine kuona tija katika sekta hiyo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here