Home KITAIFA ZANZIBAR YAJIPANGA KUFANYA MAGEUZI YA KIELIMU

ZANZIBAR YAJIPANGA KUFANYA MAGEUZI YA KIELIMU

Google search engine
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela  Mohammed  Mussa akitoa Taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na mageuzi katika sekta ya elimu huko Ofisini kwake Mazizini Mjinin Unguja.

Na FAUZIA MUSSA

-MAELEZO, ZANZIBAR

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imekusudia kufanya mageuzi ya kielimu kwa kuifanya Elimu ya amali kuwa ya lazima baada ya kukamilika kwa marekebisho ya sheria ya elimu ya mwaka 1982 na sera ya mwaka 2006.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko hayo huko Ofisini kwake Mazizini Waziri wa Wizara hiyo, Lela Mohammed Mussa amesema mabadiliko hayo itasaidia wanafunzi kuwa na ujuzi na maarifa watakapomaliza masomo yao.

Aidha amesema hatua hiyo inafanyika kufuatia mabadiliko ya mtaala wa elimu ya maandalizi na msingi ulioanza kutumika mwaka huu wenye lengo la kuwafanya wanafunzi wanaomaliza  kidato cha pili kuendelea na elimu yao katika madarasa ya amali.

Vilevile Wizara inakusudia kufuta mitihani ya Taifa ya Darasa la nne na la kumi baada ya kuona matokeo mazuri ya utekelezaji wa mtaala mpya wa ujenzi wa umahiri.

Waziri Lela amesema Wizara inakusudia kuweka  miundombinu ya TEHAMA katika Skuli zote ili kuwezesha maendeleo ya kidijitali na kuimarisha Tehama na ubunifu katika elimu pamoja na kuanzisha program za ufundi za TEHAMA ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa  kompyuta,simu  za mkononi pamoja na biashara ya mitandao ya kijamii.

Alifahamisha kuwa katika kuboresha mazingira ya elimu Wizara inakusudia kuanzisha dahalia za michepuo katika Wilaya zote ambazo zitapelekea mchanganyiko wa wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali na kuimarisha usawa wa utoaji wa huduma za elimu.

Google search engine
Previous articleSERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA 5,000 MSOMERA NDANI YA MIEZI SITA
Next articleMSD KUGAWA VYANDARUA 700,000 SHULE ZOTE DAR, RC CHALAMILA ATAKA UPULIZAJI DAWA KUUA MAZALIA YA MBU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here