Home MICHEZO BASATA VIBES KUTIKISA MIKOA YOTE NCHINI

BASATA VIBES KUTIKISA MIKOA YOTE NCHINI

Google search engine
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro, akizungumza kwenye uzinduzi huo leo Septemba 14, Jijini Dar es Salaam

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lihakikishe kuwa Mradi wa Baraza hilo ujulikanao kama BASATA Vibes unawafikia Wasanii mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ili azma ya Serikali ya kukuza sanaa nchini itimie.

Dk. Ndumbaro ametoa agizo hilo leo Septamba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Mradi wa BASATA Vibes na Kituo cha Utamaduni Cha Ufaransa hapa nchini wenye lengo la kuimarisha maonesho ya Sanaa, kutoa mafunzo kwa Wadau wa Sanaa na kuwajengea uwezo wa kuandaa matukio ya burudani.

” Kupitia Ubalozi wa Ufaransa natumia nafasi hii kwenu Ubalozi kuhakikisha mashindano ya michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024 uhusishe burudani kutoka kwa wasanii wetu, hili naomba mlizingatie sana, pia katika mashindano hayo naomba mhakikishe Watanzania wanapata nafasi za kutosha kwenye michezo hiyo kwakua vigezo vya kushiriki wanavyo” amesisitiza Dk. Ndumbaro.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema kuwa atahakikisha jukumu alilokabidhiwa na Waziri la kuwapata Wanamuziki Wazuri na wenye sifa ya kuburudisha katika mashindano hayo linatimia .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Dk. Emmanuel Ishengoma akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema Sekta hiyo inatoa fursa kwa Wadau wake kupata nafasi katika soko la Kimataifa.

Aidha, Mkurugenzi wa Kituo hicho Flora Valleur amesema mradi huo pia utahusisha kujifunza Lugha la Kifaransa, na kupata nafasi kwa wasanii wa Tanzania kuhudhuria na kutoa burudani kwenye majukwaa ya burudani ya nchi hiyo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here