Home KITAIFA RAIS SAMIA AWAPA SOMO VIONGOZI AFRIKA UMUHIMU UWEKEZAJI KWENYE KILIMO BIASHARA

RAIS SAMIA AWAPA SOMO VIONGOZI AFRIKA UMUHIMU UWEKEZAJI KWENYE KILIMO BIASHARA

Google search engine
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassana akihutubia mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) ambapo marais mbalimbali wa nchi Afrika wamehudhuria mkutano huo wenye lengo la kujadili juu ya nini kifanyike kuboresha mifumo ya chakula Afrika
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye mkutano mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) huku kiwa na marais kutoa nchi mbalimbali za Afrika kulia ni Rais wa Burundi Everiste Ndayishimiye na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi na kushoto ni Rais wa Senegal Macky Sall pamoja na Rai wa Kenya, William Ruto

NA MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan, amewakubusha viongozi wa Afrika kuendelea kuwekeza katika kilimo biashara ili kulinusuru Bara la Afrika kukumbwa na uhaba wa chakula.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa tafiti mbalimbali zineonyesha kwamba asilimia 65 ya ardhi Afrika inafaa kwa kilimo.

Hayo ameyasema leo Septemba 7, 2023,  jijini Dar es Salaam, alipokuwa akihutubia mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) ambapo marais mbalimbali wa nchi Afrika wamehudhuria mkutano huo wenye lengo la kujadili juu ya nini kifanyike kuboresha mifumo ya chakula Afrika.

Amesema Jukwaa la AGRF litatoa na suluhu ya changamoto ya chakula ambapo viongozi wa Afrika wapo tayari kuhakikisha Afrika inajitosheleza kwa chakula na dunia kwa ujumla.

“Asilimia 60 ni vijana ambao ni nguvu kazi na sisi viongozi wa Afrika tupo tayari kuondoa aibu ya Afrika kuwa walalamikaji tupo tayari kulisha Afrika na duniani kwa ujumla,” amesema Dk. Samia.

Licha ya rasilimali zilizopo Afrika, Dk. Samia amesema kuwa vijana wa nchi za Afrika, wamebaki kuwa walalamikaji badala ya kutafuta suluhisho kuelekea njia ya mapinduzi ya uchumi wa kijani.

“Tupo na AGRF washiriki wa maendeleo sekta binafsi wasomi na wataalamu kubadilishana uzoefu namna ya kuboresha mnyororo wa thamani ya bidhaa za kilimo na kujadili mipango ya kuimarisha usalama wa Chakula Afrika,”amesema.

Dk. Samia, amesema kuelekea mageuzi wanayotaka katika sekta ya kilimo ni muhimu viongozi kwa pamoja tukaweka mipango na mikakati kufikia Afrika tunayoitaka.

“Ili kufikia malengo sisi viongozi wa nchi za Afrika hatuna budi kufanya tathimini ya vipaumbele vyetu na kuvioanisha na mahitaji ya sasa katika muktadha wa dunia ambapo inaelezwa kuwa zaidi ya watu milioni 283 wanalala njaa barani Afrika,” amesema  

Kwa upande wake Rais wa Kenya, William Ruto amesema ardhi ya kilimo ipo Afrika mkutano huo wa AGRF ni somo kubwa hivyo Teknolojia na muda unahitajika ili kuweza kupata chakula cha kutosha kwenye bara la Afrika hata kupeleka Duniani.

“Tunaweza kuchochea biashara ya kilimo kuacha kuwa watu wa kulalamika wakati ardhi tunayo ni suala la kuongeza uzalishaji na kufikiria tunafanyeje wakulima wazalishe zaidi,” amesema Rais Ruto.

Kutokana na hali hiyo, amesema kuwa katika somo la mkutano huo wa AGRF ni jinsi gani watafanya mabadiliko ili kubadilisha wakulima waweze kuzalisha kwa wingi ili gharama za chakula zipungue.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here