Home KITAIFA STAMICO YAVUNJA REKODI YA MAPATO, YAKUSANYA BILIONI 61.1/-

STAMICO YAVUNJA REKODI YA MAPATO, YAKUSANYA BILIONI 61.1/-

Google search engine

*MKURUGENZI MKUU AELEZA MIKAKATI MBIONI KUANZA KUJIENDESHA, KUANZISHA BENKI YA WACHIMBAJI

MKkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), Dk. Venance Mwasse (Katikati) akiwa na viongozi wa shirika hilo katika mkutano na Wahariri leo Agosti 28, 2023, jijini, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), Dk. Venance Mwasse , akieleza mikakati na mafanikio ya shirika hilo kwa wahariri, leo Agosti 28, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wahariri wakioshiriki mkutano wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), Dk. Venance Mwasse (hayupo pichani)
Baadhi ya watumishi wa STAMICO na whariri walioshiriki mkutano huo

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), Dk. Venance Mwasse, ametangaza rekodi mpya ya shirika hilo ikiwamo kuongeza mapato ya Sh bilioni 61.1 sawa na ongezeko la asilimia 4,425 toka mapato ya Sh bilioni 1.3.

Sasa ni wazi hatua hiyo imekwenda kuvunja rekodi za miaka miatno iliyopita hali iliyotishia kutaka kufuwa na shirika hilo na Serikali kwa kuonekana halina tija kwa Taifa.

Hayo yamebainika leo Agosti 28, 2023 katika kichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina nchini kwa kuwakutanisha Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari kwa lengo la kuelekeza mafanikio ya mashirika yaliyo chini ya Msajili wa Hazina.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa mafanikio hayo yameliwezesha shirika hilo kwa sasa kuanza kutoa gawio kwa Serikali kwani tangu lilipoasisiwa mwaka 1972 halijawahi kuvunja rekodi hiyo ya mapato yake yanatokana na uzalishaji hasa kwenye miradi mbalimbali nchini.

Akitaa sababu zilizowawezesha kufikia mafanikio hayo, Dk. Mwasse, amesema kuwa hatua hiyo imetokana na kubadili fikra, ushirikishwaji wa wafanyakazi, nidhamu pamoja na kusimamia malengo waliyojiwekea kwa kuhakikisha yanatekelezwa.

“Tulifikia mahali ikabidi tubadilike kifikira, kuna mashirika ya umma ambayo yanayotoa huduma na kuna mashirika ya umma ambayo yanatakiwa yajiendesha kibiashara. Kwa hiyo tulipoamua kujiendesha kibiashara, tukaamua sasa kwenda kuzitafuta fursa, tulipobonyeza hiyo button (kitufe) tukaona mambo yamekwenda.

“Hivyo nami kama kiongozi kwa kulitambua hili ni shirika la umma nikaona lazima tuumize vichwa, pamoja na kuongeza morali ya wafanyakazi kwa kuona wanajaliwa na mipango iwe inanyooka,” amesema Dk. Mwasse

Licha ya hiyo amesema kuwa pamoja na kuongeza nidhamu kwenye matumizi ya fedha za umma kwa kuchagua sehemu sahihi za kuweka fedha nyingi kwa kuangalia kwenye faida.

Dk. Mwasse pia amesema, wanaendelea kungeza uzalishaji wa mkaa mbadala ili kuondoa matumizi ya mkaa unaotokana na miti na matumizi ya kuni.

SHUGHULI ZA UCHORONGAJI MADINI

Akizungumzia shughuli za uchorongaji wa madini unaofanywa na STAMICO, Dk. Mwasse amesema kuwa shirika limezidi kufanya vizuri kwenye maeneo ya migodi nchini.

Amesema hayo hiyo imeleta ufanisi uliwawezesha kusaini mkataba mnono wa kuchoronga na mgodi mkubwa na Geita Gold Mine (GGML) mkoani Geita, ambao una thamani ya Sh bilioni 55.2 na ulitiwa saini Machi 27,2023.

Amesema hatua ya kusainiwa kwa mkataba huo ni uthibitisho kuwa Watanzania wanaweza kushiriki kikamilifu katika kandarasi zinatokea katika mnyororo wa thamani wa madini nchini.

Dk. Mwasse, amesema kuwa hatua hiyo imewafanya wajivunie kufanya kazi na GGM kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu mfululizo na kwa kipindi chote wamekuwa na ushirikiano mzuri.

“Haya kwetu tunayaita ni mageuze makubwa na tunaendelea kuimarisha tasnia ya uchorongaji na katika hili la miradi ya aina hii sisi (STAMICO) ni kinara,” amesema

WACHIMBAJI WADOGO

Dk, Mwasse, amesema kuwa STAMICO imejipanga kuwaendeleza na kuwarasimisha wachimbaji wadogo nchini kwa kuwawezesha kwa kupatia ujuzi na vifaa ili kurahisisha shughuli za uchimbaji nchini.

“Hapa tumeweka jicho letu la kipekee, tutaendelea kuwapa mafunzo, na kubwa zaidi tutahakikisha benki ya wachimbaji inaanzishwa ili kuondoa changamoto ya wachimbaji, mpaka sasa hivi hakuna benki ya wachimbaji. Nasi tayari tumeanza mchakato wa kuanzisha benki ambayo itakuwa mkombozi wa wachimbaji.

“Lakini pamoja na hilo kwa sasa bado wachimbaji hawa wanaendelea kuhudumiwa na benki za biashara nchini ambapo sisi STAMICO ndio dhamana yao nab ado tunaendelea mazungumzo nayo ambayo hii tunaamini italeta mapinduzi ya kweli kwenye sekta ya madini nchini,” amesema Mkurugenzi huyo wa STAMICO

Amesema kupitia mipango na mikakati thabiti ya shirika hilo wanatarajia ifikapo mwaka 2025, shirika liwe linajitegemea na kuondokana kusubiri ruzuku kutoka Serikali Kuu.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here