Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dk.Sifundo Chief Moyo wakati alipofika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, leo Agosti 28, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dk. Sifundo Chief Moyo (kulia) na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2023.