Home BIASHARA BENKI YA NMB YAJA NA MWALIMU SPESHO KWA KISHINDO

BENKI YA NMB YAJA NA MWALIMU SPESHO KWA KISHINDO

Google search engine
Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji akizungumza wakati akifungua kongamano la siku ya  Walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo,Mkuu huyu wa wilaya alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema
MKUU wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB Makao Makuu Martin Massawe akizungumza wakati wa kongamano la siku ya  Walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema
 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Ladislaus Baraka akizungumza wakati wa kongamano la siku ya  Walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji,ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema.
Baadhi ya Walimu kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Tanga wakifuatilia kwa umakini Kongamano la siku ya walimu wa Mkoa wa Tanga lililoandaliwa na Benki ya NMB na kufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini humo na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji, ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema

Na Mwandishi wetu Tanga.

BENKI ya NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa wadau wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari ambapo imekuja na huduma ya Mwalimu Spesho yenye lengo la kuwawezesha na kuwainua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa za mikopo kwaajili ya biashara, kilimo na ada.

Zaidi ya walimu 300 kutoka katika shule mbalimbali za msingi na sekondari mkoani wa Tanga wameshiriki warsha iliyoandaliwa na Benki hiyo ya NMB kanda ya Kaskazini kwa lengo la kuwapa elimu juu ya huduma na fursa mbalimbali zikiwemo elimu ya kifedha, na elimu ya bima.

Akizindua Warsha hiyo mkuu wa wilaya Tanga James Kaji ameipongeza Benki hiyo kwa kundelea kuboresha huduma zake kwa wadau wa hususan wa serikali akiwataka walimu kutumia fursa za mikopo zinazotolewa kwaajili ya kuwainua wateja wake hasa kiuchumi, kielimu , kwenye sekta ya kilimo akiwataka kuachana na mikopo umiza ambayo wamekuwa wakiipata sehemu nyinginezo.

Aidha Kaji alisema kwa kuwainua kiuchumi walimu itawasaidia pia kuwawezesha hata kiutendaji katika majukumu yao ya kiufundishaji hatua ambayo itasaidia kuwaandaa wanafunzi bora kitaaluma na maadili mema.

“Nitoe pongezi kubwa sana kwa Benki ya NMB kwa kuandaa kongamano hili kila mwaka kwa walimu imetoa msisitizo mkubwa na kuwawezesha walimu, wazo la kuwafikia walimu hususan katika kuwawezeaha kimikopo ni zuri na la kuigwa , na nyinyi walimu onyesheni jithada na uwezo wenu katika kuchangamkia na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana” 

“Walimu wengi katika shule zetu za msingi na sekondati wengi wao walikuwa wakijiingiza katika mikopo umiza ambayo imefanya wanashindwa kutekeleza majukumu yao ya kila siku lakini kwa fursa hizi zinazotolewa, na tumeshuhudia wengi wao kutokana na mikopo inayotokana na NMB wameboresha maisha yao kutokana na huduma jinsi ambavyo wameweza kuinuka kimapato na kuboresha maisha yao ya kila siku” alisema Kaji.

Awali akizungumza mkuu wa kitengo ya Bima kutoka benki ya NMB kanda ya kaskazini Martin Masawe kwa niaba ya afisa biashara na wateja binafsi amesema kuwa walimu wana nafasi kubwa ya kunufaika na huduma mbalimbali wanazozitoa huku wakiwa na lengo la kuwafikia walimu wote nchi nzima.

“Tumekuwa tukitoa elimu ya kifedha, elimu ya bima na elimu mbalimbali za kujipangilia kimaisha kwa walimu, bila mwalimu pengine sisi tusingekuwepo hapa na umuhimu wa walimu katika benki yetu ni jambo kubwa na la umuhimu sana tumekuwa tukifanya hivi kila mwaka na tumepanga kuwafikia walimu wote nchi nzima na kwa mwaka huu tunategemea kuwafikia walimu 9000 katika wilaya na mikoa mingi zaidi sambamba na kutoa elimu kwa walimu wote” alisema Massawe

“Benki ya NMB iliangalia ni kitu gani cha kipekee ambacho anaweza kupata mwalimu kutoka kwetu kwahiyo tulitengeneza masuluhisho kulingana na maisha yao ambapo tunayoa mikopo kwaajili ya elimu pale wanapotaka kujiendeleza au mtoto wake anaweza kupata mkopo wenye riba nafuu ya 9%, tunatoa mikopo ya kilimo , tunatoa pia mikopo kwaajili ya vyombo vya usafiri kwaajili ya kujiongezea kipato zaidi ya kile ambacho anakipata mwalimu” alisema Massawe

Baadhi ya walimu akiwemo Coletha Joseph na Maurus Ndunguru ambaye ni kaimu afisa elimu wa halmashauri ya jiji la Tanga wameishukuru na kuipongeza Benki hiyo kupitia mikopo na huduma ambazo wanazipata zitakazowasaidia kuwainua kiuchumi na kuwapa fursa ya kujiendeleza kimasomo na katika maisha ya kawaida.

“Tunaishukuru sana Benki ya NMB kwa kutuona na kutuletea huduma mbalimbali hasa ya mikopo ambayo itatusaidia kutuongezea kipato nje ya kazi yetu tutakwenda kuwaelimisha na wenzetu juu ya fursa hizi zinazopatikana ili waweze kuzitumia na kusaidia kuongeza kipato kwa ujumla ” alisema Coletha.

“Huduma hizi wanazozitoa benki ya NMB ni nzuri zitaboresha miasha ya walimu kwasababu tumekuwa tukizunguka sana kwenye mambo ya mikopo ambayo inaumiza wakati mwingine lakini kwa kuja kwao NMB hapa kutawasaidia sana walimu” alisema Ndunguru.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here