Home BIASHARA NMB yapeleka wafanyabiashara 10 China kutembelea Viwanda, Biashara na Masoko ya Kimataifa

NMB yapeleka wafanyabiashara 10 China kutembelea Viwanda, Biashara na Masoko ya Kimataifa

Google search engine

Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, Alex Mgeni (katikati) kwenye picha ya Pamoja na  wafanyabiashara 10 wanaokwenda mji wa Guangzhuo nchini China kwa ufadhili wa Benki ya NMB kutembelea Viwanda, Biashara na Masoko ya Kimataifa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Agosti 1, 2023. Hii ni mara ya Tatu Benki hiyo inawapa fursa wafanyabiashara kujifunza ziadi kutoka wenzao waliopo Nchi za nje (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, Alex Mgeni (katikati) akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege Editha Kassimu ambaye ni mmoja kati ya wafanyabiashara 10 wanaokwenda nchini China kwa ufadhili wa Benki ya NMB kwenda kutembelea Viwanda, Biashara na Masoko ya Kimataifa.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Agosti 1, 2023. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara NMB, Christopher Mgani. Hii ni mara ya Tatu Benki hiyo inawapa fursa wafanyabiashara kujifunza ziadi kutoka wenzao waliopo Nchi za nje (Na Mpiga Picha Wetu).

Na Mwandishi Wetu

Benki ya NMB imewaaga Wajasiriamali wadogo na wa kati 10 walioanza safari ya kujifunza ya siku tisa jijini Guangzhou, China kwa udhamini wa benki hiyo ilikijifunza mengi kutoka kwa taifa hilo ambalo limeendelea kibiashara.

Wafanyabiashara hao pamoja na mambo mengine wanatarajia kutembelea maonyesho ya biashara mbalimbali  kwaajili ya kujifunza masuala muhimu kwaajili ya biashara zao na pia kutembelea viwanda na masoko.

Akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mkuu WA Idara ya Biashara Alex Mgeni, alisema safari hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo unaolenga kuongeza thamani ya wateja wa benki hiyo huku akisisitiza kuwa safari hiyo itawapa washiriki mwanga mpya katika biashara zao.

“Kwa mara nyingine tena, benki ya NMB inawatangazia ya kuwa leo tuna kwenda kuwaaga wafanya biashara 10 ambao kwa udhamini wa benki ya NMB watasafiri kuelekea nchini China kwaajili ya kutembelea maonyesho ya biashara mbalimbali (Trade Fair) kwaajili ya  kujifunza masuala muhimu kwaajili ya biashara zao na pia kutembelea viwanda na masoko.

Tunatarajia leo (jana) mchana wataanza safari yao kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea huko Guangzhou China, watapumzika Dubai na kuondoka kwenda Guangzhou. Watawasili Jumatano Majira ya saa nne usiku ya huko China. Hivyo wataanza rasmi Alhamisi ziara yao kwa kutembelea Mangesh ya biashara,” alisema Mgeni.

Mgeni alisema kuwa Benki ya NMB inaamini kuwa safari hiyo itakuwa na manufaa makubwa sana siyo tu kwa wafanyabiashara hawa lakini pia kwa taifa kwa ujumla. 

“Sisi kama benki ya NMB tunaamini kuwa ukuaji wa biashara zao utasaidia na kuchangia pato la taifa, kuongeza ajira, hivyo ni manufaa kwetu sote,”alisema.

Mgeni alisema kuwa benki yake imekuwa ikiwapeleka wafanyabiashara kipindi cha nyuma hata kabla ya janga la korona huku akibainisha kuwa waka jana, benki yake iliwapeleka wafanyabiashsra 10 nchini Uturuki. 

“Mwaka tunatarajia kupeleka jumla ya wafanya biashara 25.  Tunaanza na hawa 10. Mwezi wa Oktoba tunapeleka wengine 15 kwenye Maonyesho maarufu ya Canton Fair yanayofanyika huko huko China,” alisema.

Wakati wa hafla hiyo, Editha Kassimu mfanyabiashara kutoka mjini Tanga ambaye ni miongoni wa wafanyabishara waliopata fursa hiyo alishukuru benki ya NMB kwa kuchangia ukuaji wa biashara yake tangu mwaka 2011.

“Nilanza NMB mwaka 2012 baada ya kufungua akaunti kwa kiwango kidogo sana. Niliweza kukopa na kununua mashine ya ushonaji kwa shilingi laki moja na elfu 40. Najivunia kuwa na NMB kwa kuwa iliwezesha kuniwezesha na sasa hivi hivi namiliki mashine za kisasa zaidi ya 20 na natoa ajira kwa vijana wet,” alisema.

Aliongeza, “Katika safari hii ya China, natarajia kujifunza zaidi hasa teknolojia mpya na vitu vipya katika utendaji wa kazi yake,” 

Alisema baada ya kurudi nchini, anatarajia kutoa uzoefu atakaoupata kwa wafanyabiashara wenzake ambao hawajapta fursa hiyo huku akiishukuru benki hiyo kwa kuendelea kujitolea kuendeleza wafanyabiashara wadogo.

Mkuu wa Idara ya Biashara  wa Benki ya Alex Mgeni aliongeza kuwa benki hiyo imeshirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China kufanikisha safari hiyo.

“Tumefurahi kuungana tena na wateja wetu siku ya leo na hii ni kuunga mkono falsafa yetu ya karibu yako. Leo ni mara ya tatu tangu tuanza zoezi kama hii. Wateja wengi ambao wanasafiri wanafanya biashara ya vifaa vya ujenzi, vipuli na biashara ya vipodozi,” alisema.

Aliongeza kuwa wateja hao watapata fursa ya kujifunza mengi kwa kuwa nchi ya China ni miongoni mwa nchi ambazo zimeendelea sana katika Nyanja hizo kwa kutumia teknolojia.

“Tunatarajia kuwa wafanyabiashara hawa watajifunza mbinu za kuzalisha kwa ubora na mafanikio zaidi na kuongeza tija katika biashara zao,” alisema.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here