Home KITAIFA Tunasajili Wanachama Sabasaba- NHIF

Tunasajili Wanachama Sabasaba- NHIF

Google search engine

Na Mwandishi Wetu

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umewahimiza wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na waliotoka katika maeneo mbalimbali nchini kufika katika Banda la NHIF katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ili kupata huduma ya kusajili kuwa wanachama.

Rai hiyo imetolewa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Anjela Mziray ambaye ameeleza kuwa, kupitia Maonesho ya 47 yanayoendelea sasa katika viwanja hivyo, Mfuko unatoa huduma ya usajili wa wanachama kupitia mpango wa Vifurushi ambao unamwezesha kila mwananchi kujiunga na kunufaika kwa kuwa na uhakika wa matibabu.

Amesema kuwa mbali na usajili wa wanachama, Mfuko pia unatumia fursa hiyo kutoa elimu ya dhana ya bima ya afya na umuhimu wa kujiunga kabla ya changamoto za afya, kupokea mrejesho wa huduma na maoni ya uboreshaji wa huduma na kushughulikia changamoto mbalimbali walizokutana nazo wanachama.

“Tuko hapa Sabasaba katika Jengo la NHIF na mwaka huu tumekuja na huduma ya usajili wa wanachama kupitia Mpango.”

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here