Home KITAIFA Changamoto viumbe vamizi yaibua mjadala kwenye sekta utalii

Changamoto viumbe vamizi yaibua mjadala kwenye sekta utalii

Google search engine
Mwenyekiti wa JET, Dk. Ellen Otaru akiongoza mjadala kuhusu uvamizi wa aina ya viumbe kwenye sekta ya utalii, kupitia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili

NA MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

IMEELEZWA kuwa hatua ya kuzorota kwa ustawi wa sekta ya utalii nchini imekuwa ikichangiwa na uwepo wa changamoto ya uvamizi kwenye uhifadhi jambo linalochangia kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Kutokana na hali hiyo kwa sasa viumbe vamizi ambao wamekuwa wakihusisha aina ya mimea, wanyama hasa kwa kiumbe ambacho kimeletwa kwa mara ya kwanza kwa kuwa vamizi hasa kinapoletea kutokea kwa uharibifu.

Hayo yamesemwa Juni 21, 2023 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kitengo cha Sera za Maliasili Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Joseph Olila, katika mjadala uliohusisha Wahariri wa vyombo vya habari uliojadili changamoto za viumbe vamizi ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET).

Meneja wa Kitengo cha Sera za Maliasili Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Joseph Olila

Kutokana na hali hiyo Olila, amesema kuwa changamoto za mazingira zinajitokeza ikiwamo kupotea kwa Baonuwai  na kusababisha spishi vamizi kuweza kuhama.

“Hii inaweza kuwa na athari kwenye mfumo ikolojia, kwani kila aina za viumbe wa asili kwani nao wana jukumu katika mnyororo wa chakula na usawa wa jumla wa mfumo.

“Uharibifu wa makazi na aina ya wanyama vamizi inaweza kubadilisha makazi, kutofaa kwa wanyama asilia kwani hii inaweza kusababisha hasara ya maeneo muhimu ya kutagia, kulisha na kuzaliana.

“Wanaweza kueneza magonjwa kwa mimea asilia na wanyama pamoja na kuharibu miundombinu, kama vile mabwawa na mifereji ya maji,” amesema Mtaalamu huyo kutoka Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili

Akizungumza changamoto za kijamii, Olila amesema kuwa aina ya viumbe vamizi wanaweza kuvuruga tamaduni za jadi na maisha pamoja na kuleta tishio kwa afya ya binadamu, kwa kueneza magonjwa au kusababisha athari za mzio ikiwamo kuharibu mali, kama vile mazao na mifugo.

“Changamoto za kiuchumi aina vamizi zinaweza kugharimu biashara na serikali mamilioni ya dola katika gharama za udhibiti na usimamizi. Wanaweza kupunguza tija ya kilimo, na hivyo kusababisha kuongezeka bei za vyakula.

“Wanaweza kuharibu tasnia ya utalii, kwani kuna uwezekano mdogo wa watu kufanya hivyo tembelea maeneo ambayo aina vamizi zipo, kuongezeka kwa gharama za huduma za afya katika ngazi ya kaya na kitaifa,” Olila

Amesema kuwa viumbe vamizi vinaweza kuharibu miundombinu, kama vile barabara, madaraja, na nyaya za umeme kwani hali hiyo inaweza kusababisha matengenezo ya gharama kubwa na usumbufu wa huduma

Akieleza mipango ya kushughulikia aina viumbe vamizi, amesema kuwa mipango kadhaa inayoendelea ya kudhibiti wadudu kwa kutumia kuzuia na kutokomeza.

“Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais -Mazingira iliratibu maendeleo ya Mkakati na Hatua ya Kitaifa ya aina vamizi Panga (2019-2029) kuzuia kuanzishwa na kuenea kwa aina mpya ya viumbe vamizi, kupunguza athari mbaya za zilizopo na zinazopewa kipaumbele, kuongeza uwezo wa kitaifa wa kusimamia na utafiti juu ya spishi vamizi na mamlaka zausimamizi wa wanyama vamizi katika zana ya udhibiti  kwa kuwa na malengo sita ya kimkakati.

“Maeneo hayo yenye viumbe vamizi yanayopewa kipaumbele ni sekta ya mifugo, ambapo pia kuna mesquite ni mti ambao uliletwa Tanzania miaka ya 1950 kwa ajili ya kudhibiti mmomonyoko ambapo tangu wakati huo nao imekuwa vamizi, kuenea kwa haraka na kuhamisha mimea asilia.

“Sekta ya misitu ni kichaka ambacho kilikuwa imetambulishwa nchini Tanzania kama mmea wa mapambo. Imekuwa tangu kuwa vamizi, na kutengeneza vichaka vizito ambavyo vinasongamana nje ya asili mimea na kuifanya iwe ngumu kupita pamoja na magugu maji, ambapo hapa sekta za maji na usafiri ndio sehemu kubwa ya waathirika wa hili.

“Kimazingira kiumbe vamizi kinatabia ya kuleta changamoto ikiwamo kuondoa viumbe vilivyokuwapo awali kwa kuchukua nafasi zao. Hii pia inasababisha uharibifu wa eneo la asili kama uoto wa asili, hivyo kwa namna moja ama nyingine viumbe vilivyopo vitaathirika.

“Kuna changamoto ya kimazingira ambapo husababisha magonjwa kwani viumbe asili vinakuwa havina kinga wala kuandaliwa kibaolojia kumudu changamoto hiyo,” amesema Olila

Meneja Ufuatiliaji kutoka Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, John Noronha

Kwa upande wake Meneja Ufuatiliaji kutoka Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, John Noronha, amesema kuwa ili kudhibiti viumbe hivyo ni vema kuhakikisha haviwezi kuingia kwenye mfumo wa uzalishaji.

“Sababu ya kuzuia kushamiri kwa viumbe hivi ni pamoja na kutokuwapo kwa viumbe ambavyo vinamtegemea kwa chakula. Pia kutoa uelewa mpana kwa jamii na wadau wengine juu ya viumbe hivi.

“Matharani kuna viumbe kama Siam Weed huyu ndiye kiumbe anayesumbua kwa kiwango kikubwa katika sekta ya wanyama nchini Tanzania, hivyo ni wajibu wetu kuendelea kutoa elimu,” amesema Noronha

Noronha amewataja baadhi ya wanayama wanaosababisha mgongano ambao ni Tembo, Simba, Fisi na wengine.

“Sambamba na hayo pia bado kuna changamoto ya upungufu wa sheria, mfano: kama wewe umelima kwenye kingo ya hifadhi basi hautafidiwa, vitu kama hivi vinapaswa kuangaliwa,” amesema.

Mhifadhi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Msafiri Kasara

Upande wake, Mhifadhi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Msafiri Kasara amesema wameendelea kutoa elimu kwa wananchi hususan walioko katika Wilaya zenye mapori hatua ambayo imesaidia kuimarisha ulinzi.

“TAWA tumeweka utaratibu kwamba asilimia 25 ya pato ambalo linapatikana katika pori linalozunguka wananchi linakuwa ni la kwao.

“Hivyo, mwananchi haoni haja ya kufanya ujangili na hadi kufikia sasa Shilingi bilioni 37 zimetumika kwa ajili ya malipo hayo, mbali na hilo tumeweka kipaumbele cha huduma muhimu kama shule, zahanati na nyingine,” amesema.

washiriki wa mjadala wa Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili

Awali akifungu mjadala huo Mwenyekiti wa JET, Dk. Ellen Otaru, amesema mafunzo ya Baonuai ni muhimu katika uhifadhi wa mazingira nchini.

“Tunafundisha jamii na kuelimisha pia kuhusu sera, lengo likiwa ni kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi katika uhifadhi wa Baonuai kupitia vyombo vya habari,” amesema Dk. Ellen.

JET imekuwa na utaratibu wa kukutana makundi mbalimbali yakiwamo ya wanahabari kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya mazingira nchini.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here