Home MICHEZO Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa...

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Google search engine
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ubungo, Shadrack Makangula akizungumza wakati wa mchezo wa kuwania kutinga fainali katika Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla, wengine waliokaa mbele ni Diwani wa Makurumla Bakari Kimwanga (mwenye miwani) Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ubungo, Nehemia Philimon pamoja na Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ubungo ambaye pia ni muandaaji wa mashindano ya rede, Hawa Abdulrahman
Wachezaji wa Timu ya Ting Wayland wakiumana uwanjani na timu ya Lamasia FC ambapo katika mchezo huo Ting wamefanikiwa kutinga fainali kwa kushinda bao 2-0
Wachezaji wa timu za rede wakiumana kuwania hatua ya fainali katika mashindano ya Hawa Abdul Rede CUP ambapo imezikutanisha Timu ya Kanuni ilishinda bao 2-0 dhidi ya timu ya Manzese Princes

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

Hekaheka za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu katika ligi ya Kimwanga CUP na mashindano ya Hawa Abdul Rede CUP yamepamba moto huku Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Ubungo, Shadrack Makangula, akiwataka vijana kutumia fursa hiyo kama sehemu ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika mtanange huo kwa upande wa mpira wa miguu umezikutanisha timu za Ting Wayland ambapo ilifanikiwa kuvuka hatua ya fainali kwa kuchambana timu cha kituo cha kulea vipaji Lamasia FC kwa bao 2-0 huku upande wa Rede timu ya Kanuni ikifanikiwa nayo kwenda fainali kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manzese Princes.

Hayo ameyasema kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayopigwa katika Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo, katika mashindano hayo ya kuwania ng’ombe aliyoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo, Bakari Kimwanga pamoja na Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Ubungo, Hawa Abdulraman ambaye amekutanisha mabinti nao kuwania ng’ombe katika michuano hiyo.

“Kwanza, nitumie nafasi hii kuwashukuru madiwani wetu kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuanzisha michuano ya mpira wa miguu na rede ambayo yote kwa ujumla wake yanawasaidia vijana wetu kuonyesha vipaji vyao walivyonavyo, lakini pia inasaidia kupata exposure (fursa)  na kubwa zaidi kutengeneza mahusiano mazuri baina ya viongozi na wananchi.

“Hivyo ni vema kwa mashabiki, wakeleketwa na wananchi kwa ujumla ambao timu zao wanazozishabikia zimefuzu kucheza nusu fainali kuhakikisha kuwa wakati wa michezo hiyo inapoendelea wawe na utulivu wawapo uwanjani kwa sababu tutakapoanzisha vurugu uwanjani hapa tutawakatisha tamaa wadau, wahisani na viongozi katika kuanzisha ligi mbalimbali kwa ujumla wake,” amesema Makangula

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amewataka wananchi kwa ujumla kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya aliwashukuru viongozi mbalimbali aliombatana nao na kuwaomba madiwani hao michezo hiyo iwe endelevu.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here