“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi.
Pole kwa familia, ndugu, jamaa & marafiki.
Mungu amweke mahali pema. Amina”
Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
====== ======= ======
Taarifa zinaeleza kuwa Mhe. Bernard Kamilius Membe amefariki Dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.
,inaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.