Home KITAIFA Rais Dk. Samia atua Windhoek nchini Namibia kwa kishindo, kuhudhuria mkutano wa...

Rais Dk. Samia atua Windhoek nchini Namibia kwa kishindo, kuhudhuria mkutano wa dharura wa Troika Plus

Google search engine
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa dharura wa Troika plus wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazochangia Vikosi kwenye Force Intervention Brigade (FIC) tarehe 07 Mei, 2023. Mkutano huo utajadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Namibia, Hage Geingob mara baada ya kuwasili Windhoek, Namibia kwa ajili ya mkutano wa Dharura wa TROIKA Plus utakaojadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tarehe 07 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Watoto Miranda Masatu wa kwanza kulia, pamoja na Samra Mdee mara baada ya kuwasili Windhoek, Namibia tarehe 07 Mei, 2023. Wa kwanza kulia ni Rais wa Namibia, Hage Geingob akishuhudia tukio hilo.
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here