Home KITAIFA LHRC watoa tamko kulaani mauaji ya Dk. Isack Sima

LHRC watoa tamko kulaani mauaji ya Dk. Isack Sima

Google search engine
Marehemu Dk. Isack Sima, enzi za uhai wake

NA ANDREW CHALE,
DAR ES SALAAM.

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimelaani na kukemea matukio ya mauaji yanayoendelea nchini kwani matukio hayo yanapoka haki ya kuishi likiwemo tukio la Dk. Isack Sima lililotokea hivi karibuni Tarime, Mkoani Mara.

Katika tamko hilo lililotolewa na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Felista Mauya imebainisha kuwa, Ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2022 imeonyesha uwepo wa matukio kadhaa ya mauaji yanayofanywa na watu mbalimbali ikiwemo watu wasiojulikana pamoja na matukio ya kujichukulia sheria mkononi.

“Mnamo tarehe 6/05/2023 LHRC kilipokea taarifa za mauaji ya Dk. Isack Sima aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Nyang’oto Kata ya Nyamongo, Tarime Mkoani Mara. 

Dk. Sima anadaiwa kuuwawa tarehe 3/05/2023 kikatili wakati akitoka kazini.Taarifa zimeeleza kuwa siku moja kabla ya mauti kumfika alishinda kazini akihudumia wagonjwa hadi usiku.

Matukio hayo yameripotiwa kutoka maeneo mbalimbali  hapa nchini ikiwemo Mkoa wa Mara.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya kikatili bali kuendelea kulinda na kuheshimu haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatoa rai kwa Jeshi letu la Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili na kuhakikisha waliofanya uhalifu huo wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.” Ilibainisha taarifa hiyo ya LHRC.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here