Home KIMATAIFA Wanahabari watatu wa Irani waliofungwa gerezani watunukiwa Tuzo ya Dunia ya Uhuru...

Wanahabari watatu wa Irani waliofungwa gerezani watunukiwa Tuzo ya Dunia ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ya UNESCO/Guillermo Cano 2023

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

Wanahabri watatu wa nchini Irani, Niloofar Hamedi, Elaheh Mohammadi na Narges Mohammadi wametajwa kuwa washindi wa Tuzo ya Dunia ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ya UNESCO/Guillermo Cano 2023, kutokana na pendekezo la Baraza la Kimataifa la Wanataaluma wa Vyombo vya Habari.

Sherehe ya Tuzo itafanyika jioni ya Mei 2 huko New York, mbele ya Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO.

Niloofar Hamedi anaandikia gazeti la kila siku la Shargh la wanamageuzi. Alitangaza habari za kifo cha Masha Amini kufuatia kuzuiliwa kwake chini ya ulinzi wa polisi Septemba 16,  2022, hadi sasa mwanahabri huyo yupo kifungoni katika Gereza la Evin la Iran tangu Septemba 2022.

Elaheh Mohammadi ambaye anaandikia gazeti la wanamageuzi, Ham-Mihan, linaloangazia masuala ya kijamii na usawa wa kijinsia. Aliripoti kuhusu mazishi ya Masha Amini, na pia amewekwa kizuizini katika Gereza la Evin tangu Septemba 2022. Hapo awali alikuwa amezuiwa kuripoti kwa mwaka mmoja katika 2020 kutokana na kazi yake.

Nao Niloofar Hamedi na Elaheh Mohammadi ni washindi wa pamoja wa Tuzo la Kimataifa la Uhuru wa Vyombo vya Habari 2023 na Wanahabari wa Kanada wa Kujieleza Huru (CJFE), na Tuzo la Harvard la 2023 la Louis M. Lyons la Dhamiri na Uadilifu katika Uandishi wa Habari. Walitajwa kuwa wawili kati ya Watu 100 Wenye Ushawishi Zaidi wa Jarida la Time la 2023.

Narges Mohammadi amefanya kazi kwa miaka mingi kama mwandishi wa habari kwa anuwai ya magazeti na pia ni mwandishi na Makamu Mkurugenzi wa asasi ya kiraia yenye makao yake Tehran ya Watetezi wa Haki za Kibinadamu Center (DHRC).

Kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 16 jela katika Gereza la Evin. Ameendelea kuripoti kwa maandishi kutoka gerezani, na pia amewahoji wafungwa wengine wanawake. Mahojiano haya yalijumuishwa katika kitabu chake “White Torture”. Mnamo 2022, alishinda Tuzo la Ujasiri la Waandishi Wasio na Mipaka (RSF).

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here