Home KIMATAIFA RC Makala awataka viongozi Majukwaa la Wanawake kuleta mabadiliko chanya kwa wanawake...

RC Makala awataka viongozi Majukwaa la Wanawake kuleta mabadiliko chanya kwa wanawake Dar es Salaam

Google search engine
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, azkizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa majukwa ya uwezeshaji kiuchumi ya wanawake ya mkoa huo leo jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, CPA Amos Makalla ameelekeza Jukwaa la Uwekezaji Wanawake Kiuchumi Mkoa huo kuja na mpango kazi wa kuleta mabadiliko chanya kwa Wanawake ikiwa ni pamoja na kuwafikia wengi zaidi ili kuleta tija na mabadiliko ya kiuchumi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo leo Mei3, 2023 wakati ufunguzi wa Mafunzo maalumu kwa viongozi wa majukwaa ya Wanawake mkoani humo ambapo ameelekeza mafunzo waliyopata wakayashushe ngazi ya wilaya, kata na mitaa ili kunufaisha wanawake wengi zaidi.

Aidha Makalla ameelekeza dhana ya uwezeshaji wanawake kiuchumi iende sambamba na kuwapatia fursa mbalimbali zinazopatikana ili kuwakwamua kiuchumi.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alilotoa kwa kila mkoa kuyalea na kuyatunza majukwaa ya wanawake.

Sanjari na hayo, CPA Makalla amewataka viongozi wa majukwaa ya wanawake kuelimisha wanawake kuhusu umuhimu wa kufanya mambo machache kwa ufanisi na tija na sio kujaribu kila biashara.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa majukwa ya wanawake kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam leo
Makatibu Tawala wa wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam, wakishiriki majunzo hayo ya majukwa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi
Washiriki wa mafunzo ya majukwa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here