Home KITAIFA Benki ya NMB kutatua changamoto upungufu wa meza, viti kwa walimu Shule...

Benki ya NMB kutatua changamoto upungufu wa meza, viti kwa walimu Shule ya Sekondari Sokoine

Google search engine
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa Benki Ya NMB, Vicky Bishubo ( kushoto) alipotembelea Banda la Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya “Mama Samia legal Aid” yenye lengo la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi hususani walio maeneo ya pembezoni. Wapili kulia ni Waziri wa Katiba na sheria, Dk. Damas Ndumbaro na wengine ni watumishi wa Benki ya NMB.

Na Mwandishi Wetu

Morogoro

Benki ya NMB ipo mbioni kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kumaliza changamoto ya upungufu wa meza na viti kwa walimu wa shule ya sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine iliyopo wilaya ya Mvomero  hali ambayo inalazimu walimu kutumia madawati ya wanafunzi katika shughuli zao za kila siku shuleni hapo.

Benki hiyo imeahidi kutoa msaada wa meza 30 na viti 30 vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4 ndani na miezi mitatu ikiwa ni dhamira yake ya kumaliza tatizo hilo.

Akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha sita wilayani hapa, Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema benki imedhamiria kuchangia maendele endelevu ya kijamii nchin kote ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa benki hiyo wa kurudisha kwa jamii inapofanyia kazi.

Nsolo alisema benki yake inatambua mchango wa serikali katika shule hiyo hivyo wao kama benki wanaunga juhudi hizo kwani wamekuwa na utaratibu wa kutenga fungu la kusaidia jamii katika sekta ya elimu, afya na majanga yanayoikumbuka kila mwaka kama sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.

“Kila mwaka benki ya NMB imekuwa ikitenga sehemu ya faida yetu baada ya kulipa kodi serikalini na mwaka huu benki imetenga kiasi cha sh6.6bilioni ambazo zinasaidia jamii katika sekta ya elimu, afya na majanga na shule hii ya Kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine tutatoa msaada wa meza 30 na viti 30 ili kumaliza tatizo la ukosefu wa meza na viti inayowalazimu walimu kutumia madawati ya wanafunzi kugeuza meza na viti katika shughuli zao za kila siku.”alisema Nsolo.

Nsolo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, amewataka wanafunzi hao kujiandaa zaidi katika mitihani ya taifa ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita huku akiwataka watakaporudi majumbani baada ya kumaliza mitihani hiyo kuwa na tabia nzuri ili wale wataochaguliwa kwenda chuo na JKT kuendeleza nidhamu, bidii na juhudi ikiwa sehemu ya kuenzi mienendo ya hayati, Edward Sokoine aliyeishi katika misingi hiyo na mingine.

Awali katika risala ya wahitimu kidato cha sita iliyosomwa na Boniface Lodovick (20) alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa mashine ya kuzalisha mitihani (Photocopy Machine na Printing Machine), uchache wa vitabu hasa kwa kidato cha tano na sita kama hesabu, uchumi, jiografia, kingereza na historia.

Kwa upande wa Mkuu wa shule hiyo, Gosbert Rwagasira alisema licha ya serikali kuwezesha mambo mengi mazuri zipo changamoto ambazo zinapaswa kutafutia ufumbuzi wa haraka kama kujengwa kwa daraja la kudumu ili wanafunzi na walimu kuondokana na adha ya kutotumia daraja la muda pindi mvua kubwa zinaponyesha daraja hilo hushindwa kutumika.

“Tunalo daraja la muda linalotenganisha kati ya mabweni, ofisi za kiutala na madarasa kwani nyakati za mvua kubwa daraja hilo halipitiki kwa sababu maji hupita juu na kwa usalama zaidi tunalazimika kuzunguka zaidi eneo hilo na kuchelewa kufika ofisini ama wanafunzi darasani kujengwa daraja la kudumu itakuwa mkombozi kwetu na ahadi ya NMB ya kutupatia meza 30 na viti 30 itaondoa changamoto pia ya walimu kutumia madawati ya wanafunzi kugeuza meza na viti.”alisema Rwegasira.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here