Home KITAIFA Waziri Ummy: Tutawapanga upya madaktari bingwa katika hospitali zote nchini, kukabiliana na...

Waziri Ummy: Tutawapanga upya madaktari bingwa katika hospitali zote nchini, kukabiliana na uhaba

Google search engine
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

NA MWANDISHI WETU, WAF

– BUNGENI DODOMA

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu leo Aprili 18, 2023 amebainisha kuwa, katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madaktari Bingwa katika baadhi ya hospitali za rufaa za mikoa, wizara imelenga kugawa upya madaktari bingwa waliopo katika hospitali ili kukabiliana dhidi ya changamoto hiyo katika maeneo ya utoaji huduma.

Hayo ameyasema Bungeni Jijini Dodoma wakati akifafanua zaidi maswali atayoulizwa na Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka, katika Mkutano wa 11 katika kikao cha tisa.

“Hatua ya haraka ambayo tumeifanya, tumefanya tathimini ya madaktari bingwa, tumegundua baadhi ya hospitali za rufaa za mikoa kuna madaktari bingwa wengi kuliko baadhi ya hospitali nyingine, kwahiyo tunafanya ugawaji upya ili kukidhi mahitaji katika kila hospitali wakati tunasubiri walioenda kisoma,” amesema Ummy

Ameendelea kusema kuwa, mwaka huu wizara imepata kibali kipya cha ajira, hivyo imelenga kuajiri madaktari bingwa na kuwasambaza katika hospitali za Rufaa za Mikoa hasa zile zenye changamoto ya upungufu ili kukabiliana dhidi ya changamoto hiyo wa Wataalamu.

Aidha, Waziri Ummy amesema Serikali inaendelea na mkakati wa kusomesha wataalamu kwa mfumo wa kujiendeleza katika fani za kibingwa na wanapomaliza wanarudi katika vituo vyao ili kuendelea na majukumu yao ya kuwahudumia wananchi.

Amesema, Serikali ya Rais Samia imetenga zaidi ya Sh  bilioni 8 kwa ajili ya kwaajili ya utekelezaji wa mpango wa “Samia Suluhu Super Specialists Programu” utaosomesha madaktari bingwa zaidi ya 400 ndani na nje ya nchi utaosomesha wataalamu hao kwa muundo wa jumuhishi yaani daktari bingwa, muuguzi, mtaalamu wa usingizi.

Naye, Naibu Waziri wa Afya Dk.  Godwin Mollel akijibu juu ya uhaba wa madaktari bingwa katika hospitali ya Kitete Tabora amesema Wizara imepeleka kusoma jumla ya madaktari sita, kutoka hospitali hiyo ambao madaktari wawili  (2) wanasomea ubingwa wa magonjwa ya ndani, daktari wa magonjwa ya Kinywa, Sikio  na Koo mmoja, Mionzi mmoja, magonjwa ya dharura mmoja, na daktari bingwa wa Afya ya akina mama na uzazi mmoja.

Sambamba na hiyo, Dk. Mollel amesema, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete hadi sasa ina jumla ya madaktari bingwa watano, ambapo daktari bingwa wa Afya ya akina mama na uzazi mmoja, madaktari bingwa wa watoto watatu  na Daktari bingwa wa upasuaji mmoja.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here