Home KITAIFA Nimrod Mkono afariki dunia na siri nzito

Nimrod Mkono afariki dunia na siri nzito

Google search engine
Marehemu Nimrod Mkono

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR

Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na baadae Butiama, Nimrod Mkono (80), amefariki dunia asubuhi ya leo nchini Marekani.

Mkono alikuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), na baadaye Butiama kuanzia mwaka 2000. Mwaka 2015 alishinda ubunge kwa mara nyingine, lakini tangu mwaka 2016 yuko nchini Marekani kwa matibabu.

Mbali na hilo alikuwa anamiliki Kampuni ya Uwakili ya Mkono & Company Advocates, ambayo ilikuwa ikiendesha kesi mbalimbali ikiwamo kusimia kesi zilizokuwa chini ya Shirika ya Umeme Tanzania (Tanesco).

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu ambaye alinukuliwa na chombo kimojawapo cha habari si Best Media, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kifo cha kaka yake.

“Nimepewa taarifa na shemeji (mke wa marehemu) kwamba mzee amefariki nimempigia shemeji ameshindwa kuongea vizuri. Mzee aliondoka nchini tangu mwaka 2018 akaelekea Marekani kwa matibabu kwa sababu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kusahausahau.

“Mimi nipo Tanzania kwa sasa ninachoweza kuthibitisha ni kwamba kweli amefariki taarifa zaidi za kama alikuwa hospitali au amefariki ghafla hizo bado sijajua, nitawapa taarifa zaidi baadae,” amesema Zadock

Mkono ni nani?

Nimrod Elireheemah Mkono, alizaliwa Agosti 18, 1943 katika kijiji cha Busegwe alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini alianza ubunge mwaka 2000-2015.

Nimrod Mkono ni mwana maendeleo kwa sababu amejenga shule nyingi baadhi ya shule ni Chief Ihunyo iliyopo Kijiji cha Busegwe, Shule ya Msingi Busegwe, Chief Wanzagi, Chief Oswald Mang’ombe, Shule ya Sekondari Butuguri.

Misukosuko

Wakati wa uhai wake moja ya nyumba ya makazi ya mwanasheria huyo ambaye pia alikuwa mwanasiasa nguli nchini, Nimrod Mkono, ilitangazwa kupigwa mnada ili kulipa madeni.

Mara kadhaa Mkono amezushiwa kifo kupitia mitandao ya kijamii ambapo tukio la kwanza ilikuwa mwaka 2020 jambo ambalo lilikanushwa na familia yake.

Mbali na hilo pia kupitia kampuni zake alijikuta ofisi zake zinafungwa kwa kufungwa mnyororo kutokana na kile kilichoelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kudai kuwa anadaiwa kodi ambapo baada ya muda zilifunguliwa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here