Home KITAIFA Profesa Kitila afuturisha wananchi wake Ubungo

Profesa Kitila afuturisha wananchi wake Ubungo

Google search engine
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, akiwa na Sheikh wa Wilaya ya Ubungo, Maulid Kidebe (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata wa wilaya hiyo, Sheikh Juma Isondo, wakati wa Iftari aliyoandaa kwa ajili ya wananchi wake iliyofanyika Aprili 16, 2023 katika ukumbi wa Lion Hotel Sinza jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

-BEST MEDIA, DAR

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, amewataka Watanzania waendelee kuliombea Taifa pamoja na kumuombea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuendelea kuliletea Taifa maendeleo ya kweli wakati wote.

Hayo ameyasema leo Aprili 16, 2013 katika hafla ya Iftar aliyoiandaa kwa wananchi wa Jimbo lake katika kuendelea kuuenzi mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo amesema ni lazima viongozi wa dini waendelee kumuombea mkuu wa nchi pamoja na wasaidizi wake wakati wote ili waendelee kuileta neema nchi na Watanzania kwa ujumla.

“Mkimuombea dua Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa na utulivu nasi wasaidizi wake tunakuwa na utulivu wakati wote katika kuhakikisha tunasimamia shughuli za maendeleo katika Taifa letu na watu wake. kubwa kwangu leo sio siku ya hotuba mengi masheikh wameyashayasema. Nami naendelea kuwaomba tuendele kushikamana wakati wote.

“Huyu Sheikh Kidebe (sheikh wa wilaya) tumekuwa nyakati zote tunashirikiana na jambo kama hili tulilifanya mwaka jana na tunaendelea nyakati zote kubwa tu tuendele kuombea dua za heri ndugu zangu,” amesema Kitila

Awali Sheikh wa Wilaya ya Ubungo, Maulid Kidebe, amesema kuwa Waislamu katika wilaya hiyo wakati wote wamekuwa wakimuombea dua mbunge huyo kwani amekuwa kiongozi wa mfano na nyakati zote amekuwa karibu na wananchi wa makundi yote na dini zote.

“Sie Waislamu tunasema kwa dhati kabisa tunampenda Profesa Kitila kwani nyakati zote tumekuwa tukishirikiana naye. Hata ya mchakato wake mwaka 2020 alikuja tukazungumza na mwisho tulimuomba na kumwambia jambo wewe ni wa dini nyingine tunakuomba ukae hapa tukuombee dua na alifanya hivyo.

“Kama watu watasema napiga kampeni mie hata sijali na ninawaomba masheikh wa kata na jumuiya za Bakwata katika wilaya yetu tuendelee kumtumia Profesa Kitila ni Lulu kwetu kwani tumeshuhudia kasi kubwa ya maendeleo katika jimbo lake na pia tunafuatilia michango yake bungeni ni kweli inakwenda kumgusa mwananchi wa kawaida na anajua kazi iliyompeleka bungeni,” amesema Sheikh Kidebe

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Makurumla, Idd Towatowa, akifurahi jambo na Sheikh wa Wilaya ya Ubungo Maulid Kidebe
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here