Home MAKALA Tutamwambia mama’ Ripoti hii ya CAG hakika mchelea mwana kulia….

Tutamwambia mama’ Ripoti hii ya CAG hakika mchelea mwana kulia….

Google search engine

‘Tutamwambia mama’

Ripoti hii ya CAG hakika mchelea mwana kulia….

Na Mwandishi Wetu

-BEST MEDIA

KWA sasa Watanzania wamekuwa wakisikia kauli mbalimbali tangu ilipowasilishwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wapo wanaokwenda mbali na kufanya uchambuzi wa kina ikiwa suala la wizi wa kutisha wa mali za wanyonge.

Katika ripoti hiyo yam waka 2021/22 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kicheere, aliweka wazi namna jicho lake lilivyotumia jicho katika maeneo kadhaa  akiwa yeye ndiye jicho la Bunge na Watanzania kwa ujumla.

Wakati wa kukabidhiwa kwa ripoti hiyo hivi karibuni, Taifa lilimshuhudia mkuu wa nchi, akikerekwa hadharani nah atua ya aongezeko pasi na maelezo juu ya gharama ya ndege mpya ya mizigo ambayo serikali imeagiza kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Kutokana na hali hiyo Rais Samia alisema kuwa gharama ya awali iliyokubalika ilikuwa ni dola milioni 37 serikali ililetewa bili ya dola milioni 86.

“Invoice imekuja tunatakiwa kulipa dola milioni 86. Unauliza mkataba ulisemaje? Hii imetokea wapi? Unaambiwa vifaa vimepanda bei, nauliza mkataba wetu ulisemaje? Mtu anapokea bila kuuliza anailetea serikali ilipe. Stupid,” alisema Rais Samia baada ya kupokea ripotia hiyo katika Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Kwa sababu ya ukali ulioonyeshwa hadharani na Rais, watu wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu siku ambayo ripoti hiyo itafikishwa bungeni ambako ndiko kisheria itawekwa hadharani na kuruhusiwa kujadiliwa ndani na nje ya Bunge.

Mjadala mzito umejitokeza katika mambo kadhaa ikiwamo suala la upotevu wa fedha kupitia mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu, mikataba mibovu kwenye ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kipande cha 3 na 4, hali mbaya ya Mfuko wa Bima ya Afya, gharama kubwa zisizo na sababu za utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na upotevu wa fedha katika wizara, idara, taasisi za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.

Mengi ya yaliyotajwa kwenye ripoti ya sasa yamekuwa mambo ya kawaida katika ripoti za CAG. Katika kitabu cha maisha ya CAG mstaafu, Ludovick Utouh, kiitwacho Uwajibikaji katika Kalamu Isiyo na Wino alilalamika kwamba tatizo kubwa liko kwenye ukweli kwamba mara nyingi mijadala na uchungu huonekana wakati ripoti inatoka lakini baada ya muda mfupi, Watanzania huhamia kwenye mijadala mingine na maisha kuendelea kama kawaida.

Ila tu baada ya ripotia hiyo Taifa lilimshudia Rais Samia Suluhu Hassan akichukua hatua za awali ikiwamo kuvunja bodi ya Shirika la Reli Tanzania kutokana na upotevu wa fedha katika ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR.

Naye aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amedai hakuna  uwajibika wa kutosha kutokana na mwendelezo wa ripoti zinazotolewa na idara hiyo kila Mwaka

“Mfano Ripoti ya Mwaka 2022 inaeleza kulikuwa na mapendekezo 205 yaliyotolewa Mwaka 2020, kati ya hayo 60% yamejibiwa, 40% hayakujibiwa. Inamaanisha kulikuwa na mapendekezo 82 hayakujibiwa na hatupewi taarifa yaliishiaje.”

“Mfano suala la kusema ‘Linaendelea kutekelezwa’ lina ukakasi, ripoti inapotoka kunakuwa na miaka miwili nyuma ya ukaguzi, hivyo jumla kunakuwa kama kuna miaka mitatu hapo kati, sasa inakuwaje jambo linaendelea kutekelezwa kwa miaka mitatu?”

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, CAG anatakiwa kukabidhi ripoti za hesabu zilizokaguliwa za Serikali bungeni kila mwaka kwa ajili ya kujadiliwa na kuchukuliwa kwa hatua. Katika kipindi cha walau miaka 15 iliyopita, ripoti hii imekuwa chanzo cha mijadala mikali ya kisiasa nchini humo.

Mjadala wa mwaka huu ya 2021/2022 ni muhimu katika utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa vile hii inachukuliwa kama ripoti ya kwanza ya utawala wake ya mwaka 2020/2021 iliandaliwa zaidi kwenye siku za mwisho za utawala wa mtangulizi wake, hayati John Magufuli.

Ni wazi kwamba Tanzania haiwezi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kama wabadhirifu, wazembe, wasiofuata sheria na kanuni wataachwa waendelee kufanya utaratibu wao kwa mazoea wakitegemea watalindwa na viongozi walio madarakani.

Watanzania wangependa hasa kwa Rais Samia Suluhu Hassan akutofumbia macho ubadhirifu wa rasilimali za umma kwakuwa ndiyo chanzo cha kukosekana kwa vyumba vya madarasa, mishahara midogo, vitabu, dawa katika zahhanati na hospitali na huduma nyingine muhimu kwa jamii.

Kama fedha za umma zitadhibitiwa hatutasikia kilio cha kukosekana kwa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, vijana, walemavu na wanawake kwenye halmashauri nyingi hapa nchini.

Hakika bado tuna wajibu wa kuendelea kumshauri Mkuu wetu wa nchi Rais Samia Suluhu Hassan japo ndani ya Bunge kumekuwa na mnyukano mkali kuhusu ripoti hiyo ya CAG na baadhi ya wabunge wakitaka hatua zaidi zichukuliwa ikiwamo hata kuwawajibisha baadhi ya mawaziri ambao wizara zao zimetajwa kwenye ripoti ya mwaka huu.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here