Home KITAIFA Mfumo wa Benki Wakala wachangia kukuza biashara ya bima nchini

Mfumo wa Benki Wakala wachangia kukuza biashara ya bima nchini

Google search engine
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, akijibu swali bungeni jijini Dodoma

Na. Farida Ramadhani WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Mfumo wa Benkiwakala wa Bima umesaidia kukuza biashara ya Bima nchini.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Edward Kalogeris aliyetaka kujua kama Serikali haioni kuwa kuruhusu Benki kuwa Wakala wa Bima, Mawakala wengine watafunga biashara kwa kukosa wateja.

Dk. Nchemba alisema Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na wadau wa bima ilianzisha Benkiwakala wa Bima ili kuongeza wigo wa usambazaji na upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi.

“Idadi ya Wakala wa Bima wa Kawaida imekuwa ikiongezeka sambamba na Benkiwakala wa Bima kwa sababu hali hii imechochea ushindani, ubunifu na kutegemeana”, alibainisha Dk. Nchemba.

Alisema Takwimu zinaonesha Benkiwakala waliosajiliwa ni 14 (2020), 23 (2021), 27 (2022) na 30 hadi Machi 2023 huku Wakala wa Bima wa Kawaida waliosajiliwa ni 745 (2020), 789 (2021), 910 (2022) na 960 kati ya Julai 2022 na Machi 2023.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here