Home KITAIFA BODI YA DAWASA YAPONGEZA MAENDELEO YA MRADI WA UZALISHAJI UMEME JNHPP

BODI YA DAWASA YAPONGEZA MAENDELEO YA MRADI WA UZALISHAJI UMEME JNHPP

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-RUFIJI

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), imepongeza maendeleo ya utekelezaji ujenzi  mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati 2,115 uliofikia asilimia 81.82 hadi kufikia Januari 31, 2023.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA, Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa ziara ya kutembelea  mradi wa Julius Nyerere ikiwa ni kitekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia  Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akizindua  ujazaji maji kwenye bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

“Mhe. Rais alituagiza sisi DAWASA tunufaike kupitia maji ya mto Rufiji kwa kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani baada ya kuwa yamezalisha umeme,”amesema Jenerali Mwamunyange.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amepongeza kazi nzuri iliyofanyika kwenye mradi huo  na amefurahi  ushirikiano  mkubwa uliopo kati yao (DAWASA) na TANESCO

Awali Mhandisi Mkazi Lutengano Mwandambo alieleza kuwa zoezi la ujazaji maji linaendelea vizuri na limefikia mita za  ujazo 131.02 kutoka usawa wa bahari.

Matukio mbalimbali katika picha wakati Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA ilipotembelea mradi wa kimkakati wa Julius Nyerere -JNHPP
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here