Home KIMATAIFA DRC: WANAJESHI SABA WAHUKUMIWA KIFO KWA ‘UOGA’

DRC: WANAJESHI SABA WAHUKUMIWA KIFO KWA ‘UOGA’

Google search engine

WANAJESHI saba wa Congo wamehukumiwa kifo kwa kuonyesha ‘uoga mbele ya adui’ na kusababisha hofu kuu walipokimbia waasi wa M23.Siku ya Alhamisi, wanajeshi hao walipitia katikati ya Sake, kilomita 25 magharibi mwa mji mkuu wa mashariki mwa Kongo wa Goma, “wakipiga risasi kiholelea, walipokuwa wakiwakimbia adui kutoka mstari wa mbele”, mwendesha mashtaka wa kijeshi alisema katika mahakama ikiendelea siku ya Jumamosi huko Sake.

Wanajeshi hao walikanusha mashtaka na mawakili wao walisema watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama, mamlaka ya mkoa wa Kivu Kaskazini ilisema.

Raia wawili waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya wakati wa tukio hilo lililosababishwa na kitendo cha askari, mwendesha mashtaka alisema huku akiwatuhumu kuwa ‘wauaji’.

Maelfu ya watu hivi majuzi wamekimbia makazi yao hadi Goma na Minova huku waasi wa M23 wakikaribia mji huo polepole kutoka Masisi magharibi.

Mnamo Novemba, mahakama ya kijeshi ya Goma iliwahukumu kifo askari watatu kwa “kukimbia vitani” wakati w amakabiliano dhidi ya M23 na kusababisha hofu miongoni mwa raia.

Adhabu za kifo bado zinatolewa nchini DR Congo lakini mara ya mwisho zilitekelezwa mwaka 2003, zinabadilishwa kwa utaratibu na kuwa kifungo cha maisha.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here