Home KIMATAIFA UGONJWA USIOJULIKANA WAUA WATU EQUATORIAL GUINEA

UGONJWA USIOJULIKANA WAUA WATU EQUATORIAL GUINEA

Google search engine

MARUFUKU ya kutotoka nje ya siku mbili yamewekwa katika jimbo la kaskazini mwa Guinea ya Ikweta, linaloitwa Kié-Ntem, baada ya watu 20 kufariki kutokana na ugonjwa ambao bado haujajulikana.

Vifo hivyo vilithibitishwa na mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Olamze, ambayo iko umbali mfupi kuvuka mpaka nchini Cameroon.

Kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya Cameroon, waathiriwa walipata aina fulani ya homa na kutokwa na damu puani, kuwa dhaifu, kutapika na kuhara.

Visa vya maambukizi na vifo vinatoka katika maeneo matatu kaskazini mwa Equatorial Guinea. Wanne kati ya wahasiriwa walitoka kwa familia moja.

Maambukizi hutokea kwa kuwasiliana moja kwa moja na mtu aliyeambukizwa, kulingana na mamlaka ya afya ya Cameroon.

Ndio maana wanawanawaambia watu wa Cameroon wawe makini.

Mamlaka ya Equatorial imesema kuwa mgonjwa atawekwa karantini hadi hali ya ugonjwa huo na chanzo cha mlipuko huo kuthibitishwa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here