Home KIMATAIFA IDADI YA VIFO NCHINI UTURUKI NA SYRIA YAKARIBIA 23,000

IDADI YA VIFO NCHINI UTURUKI NA SYRIA YAKARIBIA 23,000

Google search engine
Hali ya uokoaji ikiendelea nchini Uturuki. Picha na Mtandao wa BBC

IDADI ya vifo nchini Uturuki kufuatia tetemeko la ardhi la Jumatatu imeongezeka hadi 19,388, kwa mujibu wa Rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan.

Idadi ya vifo vilivyoripotiwa katika nchi jirani ya Syria inafikia 3,377, ikimaanisha kuwa jumla ya walioaga dunia imefikia karibu 23,000.

Erdogan ameongeza kuwa zaidi ya watu 77,700 wamejeruhiwa nchini Uturuki na kusema kuwa serikali itatoa msaada wa kodi kwa manusura wa tetemeko hilo.

Awali, amesema mwitikio wa serikali kuhusu tetemeko hilo la ardhi haujakuwa wa haraka kama alivyotarajia

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here