Home MICHEZO WASHINDI 100 WA BETIKA KUSHUHUDIA DABI YA SIMBA NA YANGA, APRILI 16,...

WASHINDI 100 WA BETIKA KUSHUHUDIA DABI YA SIMBA NA YANGA, APRILI 16, 2023

Google search engine
Meneja Mkazi wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betika, Tumaini Maligana akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kutangaza Kampeni ya ‘Mtoko wa Kibingwa’ ambapo washindi 100 watapata nafasi ya kushuhudia Dabi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika baina ya Simba dhidi ya Yanga.

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Betika imezindua rasmi Kampeni yake ya ‘Mtoko wa Kibingwa’ ambapo washindi 100 watapata nafasi ya kushuhudia Dabi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika baina ya Simba dhidi ya Yanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Februari 07, 2023, Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Tumaini Maligana amesema Kampeni hiyo imeanza rasmi Februari 7, 2023 na kutarajiwa kuhitimishwa rasmi April 16,2023 siku ya Dabi hiyo ya Kariakoo baina ya Watani hao wa Jadi.

Maligana amesema Kampeni hiyo ya msimu wa tano, itaendesha droo yake kila wiki na kuchukua washindi 10 hadi kukamilika kwa washindi 100 ambao watakamilisha idadi ya washindi watakaoshuhudia pambano hilo la kihistoria kwenye uwanja Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Maligana amesema: “Wateja wa Betika kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania, watapata fursa ya kutazama mchezo huo wa Simba na Yanga sanjari na kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo kusafirishwa na Ndege, kwenda na kurudi, Malazi katika Hoteli ya Nyota 5, kukaa majukwaa ya VIP uwanjani na kupelekwa uwanjani na msafara maalum.”

Aidha, Maligana ameeleza utofauti wa msimu wa tano ni kuongezeka kwa idadi kubwa ya washindi kuliko misimu iliyopita pamoja na kuwapa fursa washindi hao kushuhudia mechi hiyo kubwa inayotajwa kuwa dabi ya tatu barani Afrika.

“Kufuzu kuingia kwenye droo ya kila wiki kushinda ‘Mtoko wa Kibingwa’ unatakiwa kuweka ubashiri wako wenye Beti 5 yaani Mikeka 5 yenye dau la Tsh. 500/- na kuendelea kwa kila Mkeka, pia unaweza kuweka bashiri zako katika Ligi mbalimbali ikiwemo EPL, La Liga, Bundesliga, Serie A na Ligi ya Tanzania, unatakiwa kubeti kwa kupitia tovuti (www.bekita.co.tz) au kupitia ‘Menu’ ya kubeti ya (*149*16#),” amesema Maligana.

Meneja wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betika, Tumaini Maligana (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Afisa Mahusiano na Umma wa Kampuni hiyo, Juvenalius Rugambwa (Kushoto kwake) pembeni ni baadhi ya washindi wa Betika msimu uliopita.
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here