Home MICHEZO MWANASOKA WA GHANA AHOFIWA KUPOTEA BAADA YA TETEMEKO YA ARDHI NCHINI...

MWANASOKA WA GHANA AHOFIWA KUPOTEA BAADA YA TETEMEKO YA ARDHI NCHINI UTURUKI

Google search engine

WAFANYAKAZI wa uokoaji wanamtafuta mchezaji mpita wa miguu wa Ghana Christian Atsu, ambaye huenda amenasa chini ya vifusi baada ya tetemeko la ardhi kuikumba Uturuki.

Vyombo vya habari vya ndani vinasema mchezaji huyo wa Hataysport bado hajajulikani alipo.

Tetemeko la ardhi lilipiga sehemu za Uturuki na Syria mwendo wa saa 04:00 saa za huko (01:00 GMT) siku ya Jumatatu na lingine lilifuata baada ya muda mfupi.

Atsu alikuwa amefunga bao la ushindi kwa Hayatspor katika mechi yao ya Jumapili muda mfupi tu kabla ya tetemeko la ardhi kutokea nchini humo.

Zaidi ya watu 2,000 wamepoteza maisha nchini Uturuki na Syria baada ya matetemeko hayo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here