Home KITAIFA Sh milioni 105 zanyakuliwa droo za kila wiki NMB Mastabata

Sh milioni 105 zanyakuliwa droo za kila wiki NMB Mastabata

Google search engine

Na Mwandishi Wetu, Best Media

Droo za kila wiki za kampeni ya NMB MastaBata-Kote Kote zimetamatika jana (Ijumaa) baada ya zoezi la kuwapata washindi 76 wa mwisho kufanyika katika Manispaa ya Morogoro kwenye tawi la NMB la Wami.

Sasa imebaki droo moja ya kuwapata washindi wa zawadi ya kwanza ambayo ni safari ya mapumziko ya siku nne iliyolipiwa kila kitu huko Dubai itakayowahusisha wateja wanne pamoja na wenza wao.

Kwenye droo za kila wiki, washindi 75 wamekuwa wakinyakua Sh 100,000 kila mmoja na wa 76 akishinda pikipiki aina ya Boxer. Hii imepelekea jumla yao katika droo zote 10 za kila wiki kuwa 760.

Thamani ya zawadi walizoshinda ni pamoja na Sh milioni 75 pesa taslimu kwa washindi 750 na Sh milioni 30 za Boxer 10. Jumla ni Sh milioni 105 na thamani ya zawadi zote za shindano hili la kuchagiza malipo kidijitali ni zaidi ya Sh milioni 300.

Kabla ya zoezi la kuwapata washindi wa mwisho 76 wa kila wiki, Meneja wa Tawi la NMB Wami, Harold Lambileki, alisema droo ya kuwapata washindi wa kwenda Dubai itafanyika makao makuu ya benki hiyo wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

“Kampeni ya NMB MastaBata-Kote Kote imekuwa ni ya mafanikio makubwa sana. Baada ya droo hii ya leo, idadi ya washindi wa kila wiki itafikia 760 ambapo 750 ni wale wa Sh 100,000 kila mmoja na 10 wa pikipi,” Lambileki alibainisha.

Sokoni thamani ya kila Boxer ni takribani Sh milioni 3.

Meneja huyo alisema kila mteja wa NMB anayefanya miamala yake kwa kutumia NMB Mastercard na NMB Mastercard QR anayo nafasi ya kushinda zawadi ya safari ya Dubai huku wanaochanja sana na kulipa zaidi kidijitali wakiwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea.

Mbali na kuhamasisha matumzi ya kadi za malipo za kidijitali za NMB, kampeni za MastaBata pia zimekuwa zikilenga kuwalipa fadhila wateja na kama sehemu ya kurudisha sehemu ya faida za NMB kwa jamii.

Zawadi za MastaBata-Kote Kote zilizingatia pia kuwawezesha washindi kiuchumi. Mbali na droo 10 za kila wiki, zilifanyika droo nyingine mbili za kila mwezi ambapo washindi 98 walishinda jumla ya Sh milioni 98 na wanne piki piki.

Huu ni mwaka wa wanne wa mfululizo wa kampeni za NMB MastaBata kwa kushirikiana na kampuni ya Mastercard. Mchakato huu ulianza na MastaBata mwaka 2018, kisha MastaBata Sio Kawaida na baade MastaBata – KivyakoVyako na hii ya MastaBata-Kote Kote iliyoanza mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here