Home KITAIFA ENG RASHID KHAMSINI “MZEE WA POINT3” UJUMBE BODI YA UKURUGENZI SIMBA SC,...

ENG RASHID KHAMSINI “MZEE WA POINT3” UJUMBE BODI YA UKURUGENZI SIMBA SC, ANADI SERA MATAWINI

Google search engine

Na Andrew Chale, Best Media

Injinia Rashid Khamsini anayegombea nafasi ya ujumbe wa bodi ya Ukurugenzi katika Uchaguzi Mkuu wa Simba, amewaomba wanachama kumchagua ilikuwatimizia lengo la ushindi na kuchukua Mataji ya ubingwa.

Akiendelea kunadi sera zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Simba hapo kesho Januari 29, katika ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam, Eng. Khamsini amesema atakuwa kiunganishi muhimu cha Wanachama Mwekezaji na Wadau wa soka nchini na nje ya nchi huku akitumia kauli mbiu ya pointi tatu kila mechi.

“POINT3′ kila mechi ni mkakati wa kisera ambapo mimi mjumbe wa bodi napochaguliwa lazima tuitungie sera iwe inafanyika kivitendo na sio maneno ya porojo. Lazima tuwe na muunganiko wa viongozi na wanachama (simba nguvu moja maanake ni hii kauli) wanachama wa simba na viongozi tukiungana ndo tutaweza kuirejesha nguvu ya timu na kushinda kila mechi,”alisema Eng.Khamsini na kuongeza kuwa:

“Lazima tuwe na ‘scouting’ ya uhakika hapo nazungumzia simba sc lazima iajili seasoned technical director (mbobezi kabisa kwenye kwenye sector Hiyo mkurugenzi wa ufundi ndo kiungo cha club) Simba lazima iwe benchi la ufundi lililokuwa na wakufunzi waliobobea kwenye eneo hilo lengo kuu ni kuweka kuwapa mafunzo mazuri wachezaji na pia kuiendeleza na Simba B iweze kuzalisha wachezaji simba kubwa. Hii itasaidia kupunguza gharama za usajili na Pia itaongeza kipato klabu kwa kuuza na pia hata itakuwa chanzo kizuri kwenye timu yetu ya taifa,” alisema.

Muunganiko wa hayo machache matatu ndo msingi wa POINT3 kila mechi na silaha zengine za vita nimezificha zipo za kutosha kabisa.

Kubwa kabisa Simba bila kumfunga yanga aina maana yoyote ili simba sc wanachama tufurahi lazima tumfunge yanga na hii ni kuanzia mechi ya mwezi wa 4 wanachama wakinichagua basi yanga rasmi atafungwa goli za kutosha.

“Lazima tusimame na vision ya mwekezaji na wanachama wote tuchukue kombe la Africa na Hiyo yote inawezekana iwapo wanachama wa simba watanipa ridha na kunichagua kuwa mjumbe wa bodi.

Naombeni KURA zenu mnipigie kwa kishindo siku ya uchaguzi 29-01-2023. Nitumeni kazi kwa kukupigia KURA kwa wingi.” alimalizia Eng. Rashid Khamsini.

Hadi sasa ameweza kutembelea matawi mbali mbali ya Simba ikiwemo Dar es Salaam na Mikoani na kunadi sera zake hizo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here