Home KITAIFA RAIS SAMIA AWATAKIA HERI MEI MOSI KUANZIA DADA WA KAZI HADI DAKTARI

RAIS SAMIA AWATAKIA HERI MEI MOSI KUANZIA DADA WA KAZI HADI DAKTARI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

Kupitia ukurasa wake wa mtandao kijamii wa Instagram, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, aliwatakia heri Wafanyakazi kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa Wafanyakazi.

“Kheri ya Siku ya Wafanyakazi kwenu nyote. Siku hii ni ya mambo makubwa mawili. Jambo la kwanza ni kwa sote kuwashukuru wale ambao kwa kazi zao sisi kama Taifa tunaweza kusonga mbele; kuanzia dada wa kazi hapo nyumbani anayeamka mapema alfajiri kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, hadi daktari anayehakikisha tunapata tiba pale tunapokuwa na changamoto ya maradhi. Tunawashukuru nyote katika kila kona ya nchi yetu. Ahsanteni kwa kazi.

“Jambo la pili, leo pia ni siku ya kurudia ahadi yetu kwenu. Ahadi ambayo kila wakati tumekuwa tukiitoa na kuitekeleza kadiri tuwezavyo. Ahadi kwamba kama Serikali tutaendelea kutekeleza jukumu letu la msingi kuhakikisha mazingira ya kazi yanazidi kuwa bora zaidi kwa kila mmoja si tu mishahara, bali pia haki katika maeneo ya kazi, kupanda madaraja kwa wakati, kupata stahiki sahihi na uboreshaji wa mifumo yetu ya pensheni,” alisema Rais Samia katika ukurasa wake wa Instagram

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here