Home KIMATAIFA KIONGOZI WA UPINZANI FAYE AONGOZA MATOKEO YA URAIS SENEGAL

KIONGOZI WA UPINZANI FAYE AONGOZA MATOKEO YA URAIS SENEGAL

Google search engine
Bassirou Diomaye Faye

DAKAR, SENEGAL

KIONGOZI wa upinzani Bassirou Diomaye Faye, anaongoza katika matokeo urais nchini Senegal, huku wapinzani kadhaa wakikubali kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Mamilioni ya watu walishiriki katika upigaji kura wa amani siku ya Jumapili, bada ya miaka mitatu ya misukosuko na maandamano ya upinzani dhidi ya aliyemaliza muda wake, Macky Sall.

Wapiga kura walikuwa na chaguo la wagombea 19.

Hata hivyo, chaguo la muungano unaotawala, Amadou Ba, amekanusha ripoti za kushindwa na kusema kuwa anatazamia kushiriki katika duru ya pili ya kura ili kuamua mshindi.

Faye, mwenye umri wa miaka  44, ni mwanachama wa chama cha Pastef kinachoongozwa na Ousmane Sonko, alikuwa gerezani siku chache kabla ya uchaguzi.

Sonko aliondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa sababu ya kukutwa na hatia ya kumharibia jina.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa kwenye Televisheni yalionyesha, Faye amepata kura nyingi, na hivyo kusababisha sherehe kubwa mitaani katika Mji Mkuu wa Dakar.

Wafuasi walianza kurusha fataki, kupeperusha bendera za Senegal na kupuliza mavuvuzela.

Matokeo hayo pia yalipelekea wagombea watano wa upinzani kumtangaza Faye kuwa mshindi. Anta Babacar Ngom, mmoja wa waliotangulia, alimtakia mafanikio Bw Faye katika taarifa yake.

Sonko alimuunga mkono Faye, mwanzilishi mwenza wa chama chake kilichofutwa cha Pastef, ambaye pia alizuiliwa takriban mwaka mmoja uliopita kwa mashtaka yakiwemo ya kukashifu na kudharau mahakama.

Sheria ya msamaha iliyopitishwa mwezi huu iliruhusu kuachiliwa kwao kabla ya siku ya kupiga kura.

Wamefanya kampeni pamoja chini ya bango “Diomaye ni Sonko”. Baadhi ya wanasiasa mashuhuri na wagombeaji wa upinzani wameunga mkono kugombea kwa Faye.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here