Home KITAIFA DK. MOLLEL ATAJWA KUWA DARAJA LA MAENDELEO KWA WANANCHI WA WILAYA YA...

DK. MOLLEL ATAJWA KUWA DARAJA LA MAENDELEO KWA WANANCHI WA WILAYA YA SIHA

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-KILIMANJARO

WANANCHI wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Godwin Mollel kwa kuwa daraja la maendeleo kati ya wananchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi wa Jimbo la Siha waliojitokeza wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Siha, Dk. Godwin Mollel wakusikiliza kero za wananchi wake katika viwanja vya Rex Sanya juu Machi 19,2024 Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro

Wamesema kuwa Dk. Mollel amekuwa kiungo kizuri na imara kwenye kutatua changamoto kadha za Wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa wagonjwa wanaozuiliwa Hospitali kwa kushindwa kulipa gharama za matibabu wanazodaiwa.

Aidha wamempongeza kwa mchango wake wa hali na mali ambao umesaidia baadhi ya familia kuwatoa ndugu zao Hospitali kwa kudaiwa gharama za matibabu ambazo wameshindwa kulipa.

“Sisi wakazi wa Siha tuna kila sababu ya kukupongeza na kukuombea ili Mwenyezi Mungu aendelee kusimamia yale maono mema kwa watu wa Siha yaendelee kutimia” mwananchi ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Hata hivyo wamesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia akiwa madarakani shule mbali mbali ikiwemo shule ya wasichana ya Kilimanjaro, vituo vya Afya pamoja pamoja barabara zimejengwa na zinaendelea kujengwa pamoja na veta.

Naye Lilian Malya mmoja ya Wananchi hao amesema kupitia Dk. Mollel mtoto wake Lilian Samweli Malya

Mtoto Nickson Emanuel (7) alimpeleka kupata matibabu ya moyo katika Taasisi ya moyo ya Jakaya (JKCI) Dar esalaam ambapo alitakiwa kulipia kiasi cha Shilinhgi Milioni 22 kwa ajili ya gharama za matibabu ya mtoto huyo.

“Pamoja na kusaidia gharama za matibabu pia ameahidi kumsomesha ni jambo la kumshukuru sana na Mungu amfanyie wepesi katika majukumu yake, hizi fedha ni nyingi ni msaada mkubwa amenisaidia na aendelee kuwasaidia wengine wenye uhitaji katika jamii,” amesema Liliani.

Naye Diwani wa viti Maalumu Egger Nzao, amesema kwamba Mbunge Dk. Mollel ameweza kuwasaidia wagonjwa wengi kwa kusimamia gharama za matibabu na kuhakikisha wale watu wanatoka Hospitali

“Kwa namna ya kipekee tunampongenza anafanya kazi kubwa na aendelee kuwasaidia watu wa Siha mbali na matibabu anadhamini watoto zaidi kupata masomo ndani ya jimbo la Siha,” amesema Egger

Mbunge wa Siha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amewataka wananchi kumuunga mkono katika majukumu yake ya kuwaletea maendeleao Wakazi wa Siha.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here