Home KITAIFA UCHUMI WA TANZANIA UMEENDELEA KUHIMILI CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI ZA KIDUNIA

UCHUMI WA TANZANIA UMEENDELEA KUHIMILI CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI ZA KIDUNIA

Google search engine
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2024/2025 katika Ukumbi wa Msekwa, Bungeni Dodoma Machi 11, 2024.

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DODOMA

HALI ya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uliendelea kuhimili changamoto za kiuchumi za kidunia kama vile mabadiliko ya tabianchi na vita vya nchini Ukraine na ukanda wa Gaza pamoja na kubadilika kwa sera za fedha kwa nchi ya Marekani, ikiwemo kupandisha riba katika fedha zinawekezwa ndani ya nchi yao.

Hayo yamesemwa leo Machi 11, 2024 bungeni Jijini Dodoma  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo (MB) ameyabainisha hayo leo wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya mpango wa maendeleo ya Taifa wa mwaka 2024/2025 .

Profesa Kitila amesema Pato la Taifa liliongezeka kutoka shilingi trilioni 124.2 katika kipindi cha Januari – Septemba 2022 hadi kufikia shilingi trilioni 140.0 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba 2023. Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 liliongezeka hadi Shilingi trilioni 109.2 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba 2023 kutoka Shilingi trilioni 103.7.

“Kwa hali ya uchumi wa Taifa ulikua kwa asilimia 5.3 katika kipindi cha Januari – Septemba 2023 ukilinganisha na asilimia 5.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2022,” amesema Profesa Kitila

Waziri huyo wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, amesema kuwa ukuaji huo ulichangiwa na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo; mikakati ya kukabiliana na athari za vita kati ya Ukraine na Urusi; uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu, barabara, reli na viwanja vya ndege; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususan dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa mikopo katika sekta binafsi ambayo imechochea shughuli za kiuchumi.

Aidha Profesa Kitila amesema sekta zilizokua kwa kasi kubwa katika kipindi cha marejeo ni pamoja na: Fedha na bima (asilimia 16.0); uchimbaji madini na mawe (asilimia 10.2); umeme (asilimia 10.0); huduma nyingine ikijumuisha sanaa na burudani (asilimia 10.0); malazi na chakula (asilimia 8.9); na habari na mawasiliano (asilimia 7.9).

“Katika kipindi hicho Shughuli za uchumi zilizokuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa ni pamoja na kilimo (asilimia 24.8), ujenzi (asilimia 13.6), uchimbaji madini na mawe (asilimia 9.7), biashara na matengenezo (8.4), uchukuzi na uhifadhi wa mizigo (asilimia 7.2), na viwanda (asilimia 6.9),” amesema

Hata hivyo amesema kipindi cha mwezi Januari, 2024 mfumuko wa bei nchini ulifikia asilimia 3.0 ikilinganishwa na asilimia 4.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2023 na mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 3.8 mwaka 2023 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 4.3 mwaka 2022.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiogoza kikao cha wabunge wote leo, Machi 11, 2024 kuhusu Mpango wa Maendeleo na Ukomo wa Bajeti. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu na kulia ni Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dotto Biteko

“Kiwango hiki kipo ndani ya malengo ya kati ya asilimia 3.0 hadi 7.0. Hali hii imetokana na utekelezaji madhubuti wa sera za fedha na bajeti na kuanza kuimarika kwa upatikanaji wa mazao ya chakula katika masoko ya ndani na ya nchi jirani” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here