Home KITAIFA RAIS DK. MWINYI AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU, NAIBU MAKATIBU WAKUU ALIOWATEUA

RAIS DK. MWINYI AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU, NAIBU MAKATIBU WAKUU ALIOWATEUA

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali na Mhasibu Mkuu wa Serikali aliowateua hivi karibuni.

Uapisho huo umefanyia leo Machi 8, 2014 atika  Viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja, Zanzibar.

Walioapishwa kuwa makatibu akuu na manaibu majina na wizara zao kwenye mabano ni pamoja na  Ali Khamis Juma Katibu Mkuu )Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo), Khadija Khamis Rajab (Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ), Dk. Aboud Suleiman Jumbe Katibu Mkuu (Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale).

Wengine ni Dk. Mngereza Mzee Miraji (Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi), Fatma Mabrouk Khamis (Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda), Dk. Habiba Hassan Omar (Katibu Mkuu Wizara ya Afya), Khamis Suleiman Mwalim (Katibu Mkuu (Uchumi na Uwekezaji) Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji) na Kapteni Hamad Bakari Hamad (Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi)

Uteuzi huo pia uliwagusa Dk. Said Seif Mzee (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda), Rashid Ali Salim Naibu Katibu Mkuu (Uchumi na Uwekezaji) Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji,  Mzee Ali Haji Naibu Katibu Mkuu (Katiba na Sheria) Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Khatib Mwadini Khatib Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Pamoja na hali hiyo walioapishwa wengine ni  Omar Haji Gora Naibu Katibu Mkuu (Utumishi na Utawala Bora) Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mwanakhamis Adam Ameir Naibu Katibu Mkuu (Taaluma) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,  Mhaza Gharib Juma Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maendeleo ya Makaazi, Khalid Masoud Waziri Naibu Katibu Mkuu (Utawala) katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Dk. Mzee Suleiman Mndewa Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zahor Kassim Mohamed El Kharous Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Makame Machano Haji Naibu Katibu Mkuu (Ujenzi na Uchukuzi) Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Hamad Saleh Hamad Mhasibu Mkuu wa Serikali

Hafla hiyo ya uapisho   imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, dini na vyama vya Siasa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here