Home KITAIFA DK. TULIA AMSHUKURU RAIS SAMIA, ASEMA WANAWAKE WANAPENDANA

DK. TULIA AMSHUKURU RAIS SAMIA, ASEMA WANAWAKE WANAPENDANA

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-MBEYA

RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson, amesema kuwa Jamii inapaswa kuondoa fikra potofu kwamba Wanawake hawapendani na badala yake waige mfano wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyojitoa kwa kuwapambania na kuwapa nafasi Wanawake wenzake katika nyadhifa mbalimbali za Uongozi.

Dk. Tulia ameyasema hayo leo Novemba 13, 2023 wakati wa hafla maalum ya kumpongeza baada ya kushinda Urais wa IPU iliyoandaliwa na Chama cha Walimu Wilaya ya Mbeya Jiji iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.

Dk. Tulia amemshukuru Rais Dk. Samia kwa namna alivyohakikisha Tanzania inashinda katika Uchaguzi wa IPU uliofanyika Oktoba mwaka huu nchini Angola kwakuwa nafasi hiyo ilikuwa ni lazima nchi husika itoe ridhaa ya kutoa muwakilishi na kwa upendo wake alifanya hivyo.

Kutokana na hali hiyo, amewataka walimu wote nchini kuendelea kuweka juhudi katika kujenga taifa lililoelimika kwa kutoa elimu iliyo bora kwa Wanafunzi kwakuwa Serikali imefanya kazi kubwa kwa kuboresha mazingira ya kazi kuwa rafiki ikiwemo kulipwa madai yao mbalimbali na kwa wakati.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here